Jeshi la Polisi mkoa Morogoro limewatia mbaroni watuhumiwa wawili Maela Athanas (33) na Holo Jilia (45) wote wakazi wa Kilolero B kwa kosa la kumuua Charles Maghashi (55) mkulima mkazi wa Kilolero B .
Tukio hilo lilitokea mnamo Oktoba 29, 2023 ambapo Maela Athanas alikwenda nyumbani kwa marehemu na kumkuta amelala sebuleni kwake na kuanza kumkata na kitu chenyewe ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo chake.
Jeshi la Polisi baada ya kufanya uchunguzi limebaini kuwa, mke wa marehemu ambaye ni Holo Jilai alikula njama ya kumuua mume wake Charles Maghashi ambapo alimtuma Maela Athanas kutekeleza mauaji hayo kwa ahadi ya kumlipa pesa shilingi laki tisa (900,000) ambapo malipo ya awali alimpatia kiasi cha elfu hamsini (50,000) ili aweze kutekeleza mauaji hayo.
Aidha taarifa za mwanzo zinaeleza kuwa Holo ambaye ni mke wa
Marehemu alimtaka Mme wake waachane lakini Maghashi akikataa na ndipo Holo
alichukuwa uamzi huo wa kumuua mme wake ili apate nafasi ya kuolewa na mwanaume
mwingine.
Social Plugin