MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturuameihoji serikali ni lini itajenga vituo vya afya katika Kata ya Misughaa na Issuna ili kuweka uwiano mzuri wa wananchi kupata huduma za afya.
Mtaturu ameuliza swali hilo Novemba 7,2023,Bungeni Jijini Dodoma katika swali la msingi lililoelekezwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
“Mh Mwenyekiti,Jimbo la Singida Mashariki lina Kata 13,lakini Kata moja ndio imejengwa kituo cha afya,je ni lini serikali itajenga kituo cha afya katika kata ya Misughaa na Issuna ili kuweka uwiano mzuri katika mkakati wa afya,”.ameuliza.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri TAMISEMI Dokta Festo Dugange amesema mpango wa serikali wa kujenga vituo vya afya ni mamati endelevu.
Amesema kwa sasa serikali imeendelea kutafuta fedha kupitia mapato ya ndani ya serikali kuu na kupitia mapato ya ndani ya halmashauri na wadau mbalimbali kuhakikisha yale maeneo yaliyoainishwa ya ujenzi wa vituo vya afya kimkakati vinajengwa vituo hivyo.
“Mimi naomba nimhakikishie Mh Mtaturu kuwa nitatoa kipaumbele katika Kata alizoziainisha ili ziweze kupata vituo vya afya,”.ameahidi Dokta Dugange.
Social Plugin