Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog Shinyanga.
Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma kutoka kata ya Mwakitolyo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini amechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu maalumu kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini
Mkutano huo umefanyika leo Jumanne Novemba 28,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Chama Chamapinduzi mkoa wa Shinyanga (NSSF) kufuatia aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo Hamis Shikuba kufariki dunia mwezi Mei 22,2023 hali iliyopelekea wilaya hiyo kubaki bila na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi kwa kipindi cha zaidi ya miezi minne.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Bandora Salumu Mirambo ambaye ni Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga amemtangaza Fadhili Salmon Nyavyuma kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata kura 360 kati ya kura 398 zilizopigwa na kuwashinda washindani wake Angelina Maganga aliyepata kura 3 na Pastory Simion aliyepata kura 27.
Bandora amesema kuwa kati ya kura 398 kura 390 ni kura halali na kura zilizoharibika ni kura 8 ambapo amewashukuru wapiga kura kwa kutimiza haki yao ya msingi kwa kumchagua kiongozi atakayewaletea maendeleo katika jumuiya ya wazazi na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla.
Akitoa shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Fadhili Salmoni Nyavyuma amewashukuru wajumbe kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo huku akiahidi kuimarisha jumuiya hiyo kwa kuanzisha mradi wa mbuzi kila kata ili mbuzi hao watakapozaa waweze kusambazwa kwenye matawi ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uchumi wa jumuiya hiyo.
Pia Nyavyuma ameahidi kufanya ziara ya kutembelea kata na matawi yote ili waweze kujadiliana namna ya kuchochea maendeleo ya jumuiya ya wazazi na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi Wa mwenyekiti jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Bandora Salmu ambaye ni Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa akitangaza matokeo ya uchaguzi.
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa mwenyekiti jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini .Msimamizi mkuu wa uchaguzi Wa mwenyekiti jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Bandora Salum akiwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela (kushoto).Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma baada ya kuchaguliwa kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Katibu Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini Erenestina Richard kitoa utaratibu wa uchaguzi kwa wajumbe .
Awali wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakiwa wameketi pamoja wakisubiri kuomba kura kwa wajumbe.
Awali wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakiwa wamesimama kwa pamoja wakisubiri kuomba kura kwa wajumbe.
Katibu jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Ashura Ngade akitoa utaratibu wa uchaguzi kwa wajumbe .
Katibu jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga vijijini Ashura Ngade akitoa utaratibu wa uchaguzi kwa wajumbe
Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Wajumbe kutoka jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakisubiri kusikiliza sera za wagombea kabla ya uchaguzi.
Wajumbe kutoka jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakisubiri kusikiliza sera za wagombea kabla ya uchaguzi.
Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Mchimbaji mdogo wa madini Fadhili Salmon Nyavyuma akiomba kura kwa wajumbe nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Wajumbe wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini wakijiandaa kupiga kura
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea .
Social Plugin