Wafanyakazi wa benk ya CRDB kutoka matawi ya Mbogwe,Kahama,Tinde ,Maganzo na Shinyanga wamekutana pamoja katika ukumbi wa Shypark Hotel mjini Shinyanga kwa lengo la kusherehekea na kudumisha umoja na mshikamano baina ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Akifungua
Sherehe hiyo Meneja Rasilimali watu kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi
Benjamin Ngayiwa amesema lengo la kukutana pamoja katika ukumbi huo ni
kutaka kubadilishana mawazo ikiwa ni pamoja na kudumisha umoja na mshikamano
baina ya wafanya kazi wanaofanya kazi na benki hiyo mkoa wa Shinyanga.
Aidha
Ngayiwa ameeleza kuwa kufanyika kwa aherehe hiyo ni pamoja na utekelezaji wa
maagizo yaliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa Rasilimali watu kutoka Benki ya CRDB
makao makuu Godfrey Butasingwa kuwataka Mamenwja rasilimali watu kuandaa sherehe
itakayo wakutanisha wafanyakazi wa benki hiyo na kufurahi pamoja.
Kwa upande
wake Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana amewataka
wafanyakazi wa benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga kufurahia kwa pamoja huku
wakitafakari namna watakavyoendelea kufanya vizuri katika utendaji kazi wao
ili kanda ya Magharibi iendelee kufanya vizuri katika kanda zote za CRDB Nchini.
Costansia
Albinus ni meneja wa Bank ya CRDB Tawi la Maganzo wilaya ya Kishapu na Erick
Chambwenenge meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kahama wameushukuru uongozi wa
Kanda kwa kuandaa Sherehe hiyo maana kufanyika kwa sherehe hiyo kutakuwa ni
chachu ya kuchochea Benki ya CRDB kufanya vizuri katika matawi yao na Kanda
kwa ujumla.
Sherehe hiyo
imejumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa bao,mchezo wa Draft ,mchezo
wa karata ,mchezo wa rede kwa wanawake na michezo mingine ambapo washindi wa
michezo hiyo wameondoka na zawadi mbalimbali .
Luther Mneney Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Shinyanga akifanya utambulisho wa wafanyakazi wa Tawi hilo.
Luther Mneney Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Shinyanga akifanya utambulisho wa wafanyakazi wa Tawi hilo.
Social Plugin