MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI CHONGOLEANI TANGA NI MUHIMU KWA WATANZANIA
Tuesday, November 14, 2023
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt David Mathayo katikati akiwa na ujumbe wake wakitembelea eneo la Mradi wa Bomba la Mafuta Chongoleani Jijini Tanga wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Athumani Mbutuka
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Athumani Mbutuka akizungumza
Meneja wa eneo la mradi Mathiew Fayel akielezea jambo wakati wa ziara hiyo
Meneja wa eneo la mradi Mathiew Fayel akiwaonyesha kitu wajumbe wa kamati hiyo
Na Oscar Assenga,TANGA
MWENYEKITI wa Kamati ya kudumu ya Nishati na Madini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt David Mathayo amesema kwamba mradi wa Bomba la Mafuta kutoka hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania ni wa muhimu kwa watanzania,ueendelee na hauna madhara katika mradi huo hasa yale ya kimazingira.
Dkt Mathayo aliyasema hayo wakati kamati hiyo iliyopo kwenye ziara ya siku mbili ambapo ilitembelea katika eneo la Chongoleani na kukagua mradi wa bomba la mafuta toka Hoima nchini Uganda hadi Tanga ambapo mafuta ghafi yatasafirishwa kwenda nje ya Nchi
Alisema kwamba wanampongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kuhakikisha mradi huo unakwenda vizuri na ifikapo mwezi Desemba mwaka 2025 uwe umekamilika na kazi ya kuanza kusafirisha mafuta ghafi ianze.
“Kwa kweli tumpongeze Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kuhakikisha mradi huu unakwenda vizuri na ifikapo Desemba mwaka 2025 uwe umekamilika na kazi ya kuanza kusafirisha mafuta ghafi iianza huu mradi ni wa muhimu sana “Alisema
Alisema kwamba Bunge la Tanzania kupitia kamati hiyo inakanusha uvumi unaoenezwa wa uwepo wa uharibifu wa mazingira unaotokana na utekelezaji wa mradi wa Kimataifa wa Bomba la mafuta .
Mwenyekiti huyo alisema kwamba yapo madai yanayozungumzwa huko Duniani na hata watu toka nchi za Afrika Mashariki kuwa mradi huo ni mbaya kimazingira jambo ambalo sio la kweli.
Hata hivyo alisema kwamba wanaamini watu wanaopotosha kuhusiana na madhara ya kimazingira yatokanayo na mradi huu ni watu wasioitakia mema Tanzania ikiwemo kutaka watanzania wasifaidike nao
Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo wa Kamati alisema kwamba tayari wamekwisha kutoa maelekezo kwa watekelezaji wa mradi huo EACOP kuwa wajikite katika masuala ya kijamii ikiwemo elimu,afya,maji mengineyo
Pioa aliwataka kuhakikisha wana kuwa na idadi ya watumishi toka katika eneo la mradi ambao idadi yao bado ipo chini na wapatiwe mafunzo kwa ajili ya maslahi ya utekelezaji wa miradi huo.
Awali akizungumza katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Athumani Mbutuka alisema wamefurahishwa na kazi zinazoendelea katika mradi huo na kusema kazi kubwa ya Wabunge ni kuisimamia Serikali na imetoa maelekezo ya mambo ya msingi ya kuyafanya.
Athumani ambaye alimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini Dkt Doto Biteko alisema kwamba Serikali imeyapokea maelekezo ya kamati hiyo na watahakikisha miradi yote ya maendeleo ambayo inafadhiliwa kwa dhana ya wajibu wa jamii kushiriki inaelekezwa katika maeneo yenye tija.
Alisema tayari Dola Mil 207 zimelipwa kati dola 308 kwa ajili ya hisa za Serikali ya Tanzania, ajira 4228 zimetolewa kwa Watazania ambapo sawa na asilimia 91,Makampuni na watoa huduma 146 wametoa huduma katika mradi huo na kufanikiwa kujiingizia Shs Bil 355.
Alieleza kwamba Sh,bil 35 zililipwa kupitia fidia kwa wananchi waliopitiwa na mradi huo na kuongeza kuwa Tanzania ilikuwa na jukumu la kufanya kama Serikali na wameendeleza kutekeleza majukumu na wataenda kutekeleza yote waliyoagizwa na kamati hiyo.
Hata hivyo Meneja wa eneo la mradi Mathiew Fayel alisema mradi huo unaendela vizuri na watumishi wapo katika eneo hilo la mradi kutekeleza majukumu yao kama kuandaa nguzo kwa ajili ya jeti itakapofunga meli na mategemeo mwaka 2025 mradi utakuwa umekamilika.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin