Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), baada ya kikao baina yao alipotembelea Ofisi za Wakala Novemba 7, 2023. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Athumani Mbuttuka na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dodoma, alipofika kuwatembelea na kuzungumza na Menejimenti, Novemba 7, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Makao Makuu ya Wakala hiyo, Novemba 7, 2023 ikiwa ni kikao chake cha kwanza pamoja nao tangu aliposhika wadhifa huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kilichofanyika Makao Makuu ya Wakala hiyo jijini Dodoma, Novemba 7, 2023. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Mhandisi Styden Rwebangila.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Adrophina Tutuba (kushoto), akimkabidhi Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, Mfuko wenye baadhi ya zawadi zilizotolewa na Wafanyakazi wanawake wa Wakala hiyo kama pongezi kwake akiwa ni mwanamke mwenzao kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo nyeti. Naibu Waziri alitembelea Makao Makuu ya REA jijini Dodoma, Novemba 7, 2023 na kuzungumza na Menejimenti ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aliposhika wadhifa huo.
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage (kushoto), akimkabidhi Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, baadhi ya zawadi zilizotolewa na Wafanyakazi wanawake wa Wakala hiyo kama pongezi kwake akiwa ni mwanamke mwenzao kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo nyeti. Naibu Waziri alitembelea Makao Makuu ya REA jijini Dodoma, Novemba 7, 2023 na kuzungumza na Menejimenti ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aliposhika wadhifa huo.
Social Plugin