Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA UWANJA WA NDEGE IBADAKULI - SHINYANGA ... 'UKARABATI UNAENDELEA KWA KASI'

Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC imefanya ziara ya matembezi katika Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga kujionea ukarabati na upanuzi wa uwanja huo unaoendelea kwa kasi ambapo hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 6.5.


Ziara hiyo ya matembezi imefanyika leo Novemba 29, 2024 kujionea ujenzi wa mradi huo utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 44.8.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja wa Wakala ya Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Mibara Ndirimbi amesema mpaka sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia asilimia 6.5 huku malengo yakiwa ni kufikia asilimia 9.3 ifikapo mwezi Desemba 2023.

“Mradi huu wa ukarabati wa uwanja wa ndege wa Ibadakuli mjini Shinyanga unatarajia kukamilika ndani ya miezi 18 ambapo ulianza utekelzaji Aprili 04 Mwaka huu na ifikapo tarehe 03 Oktoba 2024 utakuwa umekamilika, mpaka sasa umefikia asilimia 6.5 huku malengo yakiwa ni kufikia asilimia 9.3 ifikapo mwezi Desemba mwaka huu”, amesema Mhandisi Ndirimbi.

Amesema utekelezaji wa mradi huo unahusisha sehemu mbili za ujenzi ambapo sehemu ya kwanza ya ujenzi itahusisha miundombinu mbalilmbali ikiwemo sehemu ya kupaki na kurukia ndege (ran way) na sehemu ya pili inahusisha ujenzi wa jengo la abiria (terminal building) sambamba na mnara wa kuongozea ndege (observation tower).

“Ukarabati na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Ibadakuli mjini Shinyanga katika eneo la kuruka na kutua ndege lenye urefu wa kilomita 2.2 umefikia asilimia 50 kwa kilomita moja kukamilika mpaka sasa” ,ameongeza Mhandisi Ndirimbi.

Kwa upande wake Mhandisi wa Vifaa na ushauri wa Kampuni SMEC Mhandisi Sosthenes John Lweikiza amesema wameanza hatua ya awali ujenzi wa jengo la abiria mara baada ya kuondoa miundo mbinu ya maji na umeme iliyokuwa katika eneo hilo.

Mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga unaojengwa na Mkandarasi China Hennan International Corperation Group Co. Ltd (CHICO) na unaosimamiwa na Wakandarasi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia umeanza Aprili 4,2023 na unatarajia kukamilika ifikapo Oktoba 3,2024 (ndani miezi 18) kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB).
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Mibara Ndirimbi akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mhandisi wa Vifaa na Ushauri wa Kampuni SMEC Mhandisi Sosthenes John Lweikiza Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea kujionea ukarabati wa uwanja huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com