Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akikagua eneo la mto lililovamiwa na watu kwaajili ya makazi katika eneo la Bunju Beach alipotembelea eneo hilo leo Novemba 8,2023 Jijini Dar es Salaam.
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BARAZA la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa onyo kwa watu wote wanaokiuka taratibu za mazingira kwa kuvamia maeneo ya bonde,vyanzo vya maji,au yaliyo tengwa kwa kusudi maalumu.
Onyo hilo limetolewa leo Novemba 8,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka wakati alipotembelea eneo la bonde la mto la Bunju Beach Jijini Dar es Salaam ambalo linadaiwa kuvamiwa na makazi ya watu.
Dkt.Gwamaka amesema kuwa ni kosa kisheria kuvamia vyanzo vya maji au eneo ambalo limetengwa na serikali kwaajili ya kusudi maalumu hivyo basi amewataka wale wote ambao wamevamia katika maeneo hayo kuhama mara moja.
"Tumelikagua eneo kwa jinsi lilivyo na tumegundua ni eneo ambalo ni nyeti kimazingira, na ni eneo nyeti kwa sababu kwanza kuna mto unaotembea kwa kipindi cha mwaka mzima,lakini pembeni yake kuna ikolojia zinazohusiana na hifadhi ya mto na baadhi ya wenyeji wamekuwa wakilima mazao yao ya muda ". Amesema Dkt.Gwamaka.
Aidha Dkt,Gwamaka amesema kuwa watu wanaokiuka sheria za uhifadhi mazingira watawajibishwa kwa kuwapelekwa katika vyombo vya kisheria kwasababu sheria iko wazi kabisa ila inapindishwa kwa baadhi ya watu ambao wasiowaelewa.
"Sheria ya mazingira kile kifungu cha 57 kinazungumza kusiwe na maendelezo yeyote ndani ya mita 60 kutoka kingo za mto, lakini hapa tumeona mawe yapo hadi mita 0 kwa maana yapo ndani ya mto" Amesema.
Pamoja na hayo amesema kuwa wapimaji wa ardhi ambao ni mawakala wa serikali wanaohusika na upimaji huo watawafatilia na wakibaini ikiwa wameweka maslahi yao mbele bila kujali kwa kukiuka maadili ya kazi yao watawaripoti katika mamlaka husika.
Sanjari na hayo Dkt.Gwamaka amewapongeza wananchi wa eneo la Consolata Bunju beach kwa kutoa taarifa mapema katika mamlaka husika na kuwasihi watanzania walinde maeneo yao na vyanzo vya maji kwani maji ni uhai.
"Lindeni lindeni maeneo yote yanayovamiwa kama vyanzo vya mito wapo wenzetu ni viziwi wameweka fedha mbele,wakasahau mali na ikolojia waliyoikuta siyo mali yao, imeshushwa na Mungu kwa ajili yao na vitukuu, unapokutana na sehemu yeyote unapoona bonde limevamiwa tupeni taarifa sisi tutawashughulikia"Ameeleza Dkt. Gwamaka
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Consolata Bunju Beach Bw. Innocent Nyiratu ameishukuru NEMC kwa kuitikia wito wa malalamiko yao na ameahidi kuwa watashirikiana nao kutoa taarifa endapo ikitokea wavamizi wa eneo hilo kuja kuendeleza eneo hilo la chanzo cha mto.
Naye Bi.Sada Makaka ambaye ni mkazi wa Bunju Beach amesema walipata wasiwasi kama wakulima wa mbogamboga kwa kuhofia kukosa maji yanatokanayo na mto huo kwa ajili ya umwagiliaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akikagua eneo la mto lililovamiwa na watu kwaajili ya makazi katika eneo la Bunju Beach alipotembelea eneo hilo leo Novemba 8,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akikagua eneo la mto lililovamiwa na watu kwaajili ya makazi katika eneo la Bunju Beach alipotembelea eneo hilo leo Novemba 8,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akitazama sehemu iliyowekwa jiwe la mpaka wa kiwanja kwenye eneo la mto lililovamiwa na watu kwaajili ya makazi katika eneo la Bunju Beach alipotembelea eneo hilo leo Novemba 8,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akikagua eneo la mto lililovamiwa na watu kwaajili ya makazi katika eneo la Bunju Beach alipotembelea eneo hilo leo Novemba 8,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa mtaa wa Bunju Beach (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea eneo la mto lililovamiwa na baadhi ya watu na kutaka kufanya shughuli zao za makazi. Dkt.Gwamaka amefanya ziara hiyo leo Novemba 8,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa mtaa wa Bunju Beach mara baada ya kutembelea eneo la mto lililovamiwa na baadhi ya watu na kutaka kufanya shughuli zao za makazi. Dkt.Gwamaka amefanya ziara hiyo leo Novemba 8,2023.
(PICHA ZOTE EMMANUEL MBATILO)
Social Plugin