Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Bw. Mark Schreiner (kushoto) walipokutana katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (Unicef), Elke Wisch (kushoto) walipokutana katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akieleza jambo wakti wa kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemaja akieleza jambo wakti wa kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Bw. Mark Schreiner akieleza jambo wakati wa kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) walipokutana katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.
Na, Mwandishi Wetu: Dar es Salaam
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuwezesha vijana kutumia fursa za kiuchumi kujiletea maendeleo.
Amesema hayo, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipokutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango na Maendeleo (UNDP) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (Unicef) nchini.
Aidha, Waziri Ndalichako ameeleza kuwa Ofisi hiyo itaendelea kukuza ushirikiano na Wadau hao wa Maendeleo maendeleo katika kuendesha programu na miradi ya uwezeshaji maendeleo ya vijana sambamba na kuimarisha ustawi wa Watu wenye Ulemavu.
Vile vile, Prof. Ndalichako amepongeza wadau hao kwa namna wanavyoendelea kuchangia jitihada za Serikali za kuinua na kuimarisha ustawi wa maendeleo ya vijana kupitia Programu na miradi mbalimbali inayotekeleza hapa nchini. Sambamba na hayo amewahakikishia kuwa wadau hao Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amehamasisha wadau hao kuwezesha vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kupata ujuzi utakaowasaidia kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kujikwamua kiuchumi.
Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja amemshukuru Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kwa namna shirika hilo lilivyojitoa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika mkoani Manyara, mwaka huu 2023.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka katika ofisi hiyo.