Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBACHAWENE AITAKA TAKUKURU KUSIMAMIA MALALAMIKO YA RUSHWA NCHINI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene. 

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Rashid Hamduni. 

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene, amekiri kuwa bado yapo malalamiko mengi ya wananchi kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika ofisi za umma hali inayosababisha wengi wao kushindwa kuzifikia huduma wanazozihitaji.

Simbachawene, aeleza hayo leo November 20,2023 jijini hapa, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).

Amesema bado yapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwepo kwa rushwa katika taasisi mbalimbali hali ambayo inasababisha wananchi kukosa huduma ambazo wanazihitaji.

“Bado suala la rushwa ndogondogo ni tatizo sana kwa wananchi wetu na huko ndiko yapo malalamiko mengi ya watu kutokana na rushwa hiyo kuwanyima fursa ya kupata huduma.

“Huduma hizo ni pamoja na elimu ngazi za chini kati hadi vyuo vikuu, lakini pia huduma za afya,kodi na leseni ambako kumewekwa utaratibu mgumu na ukilitimba katika utoaji wa huduma ili tuu watu watoe rushwa ndipo wahudumiwe”amesema Simbachawene

Aidha, amesema kutokana na hali hiyo kila taasisi inatakiwa kutengeneza mkataba wa huduma kwa wateja na TAKUKURU iwe nao kama sehemu ya kufuatilia utekelezaji wake.

“Tukitoka tuu hapa tukaenda pale hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma General tukajificha mahali na kuangalia namna shughuli zinavyoendelea kama ni muhudu au daktari atakuwa anatoa huduma bora tutaona na kama kuna muhudumu ambaye atakuwa hatoi huduma bora tutabaini hivyo hizi rushwa ndogondogo zinakera sana wananchi kuliko hata hizi za ubadhirifu wa mabilioni ambayo wao hawayaoni”amesisitiza Simbachawene. 

Kadhalika, amesema TAKUKURU, inapaswa kuendeleza kushughulikia watu wote ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa nchini bila kuangalia hali zao.

“Lazima tuwashughulikie watu wote wanaojihusisha na rushwa nchini zipo rushwa zinaoekana kabla ya kukamilika kwa miradi lakini zipo ambazo zinaanza kuonekana baada ya miaka mitatu tangu kukamilika kwa mradi hivyo wahusika wote wanatakiwa kukamatwa na kuhojiwa hata kama watakuwa wamestaafu”alisema

Amesema hali hiyo itasaidia kukomesha tabia amabzo zimeluwa zikifanywa na watumishi wa umma kujihusisha narushwa na kuhama kituo cha kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Rashid Hamduni alisema, mkutano huo ni wa siku tatu ambapo lengo lake ni kujadili mafaniko na changamoto kwa mwaka uliopita ili kuzipatia suluhu.

Amesema katika kipindi cha mwaka uliopita taasisi hiyo, imeokoa kiasi cha Sh. bilioni 171.9 ambazo zingeingia mifukoni mwa watu kama TAKUKURU, isingefanya oparesheni mbalimbali kwenye miradi ya umma.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com