Tuliuanganisha nguvu kupitia chombo tulichokiita FemAct, Kupitia nguvu na sauti ya pamoja, tuliunganisha nguvu kupaaza sauti na kuitaka sheria maalum ya kutokomeza vitendo vya udahlilishaji na Ukatili wa kijinsia kwa wanawake. Tukaamua tuipiganie sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya SOSPA ya mwaka 1998, Ujenzi wa Nguvu ya pamoja uliweza kusababisha matokeo ya sheria ile kupitishwa wakati ule.
Vijana wengi hawajui historia ya hii sheria na ni kwanini tuliidai na tukafanikisha uwepo wake. Tulifanya mambo mengi kama TAPO. Tulijenga nguvu ya pamoja, Tamwa tulipewa nafasi ya kujenga kama shirika kiongozi kwenye hii harakati. Zamani kosa la kujiamiana kinyume cha utaratibu halikuwa kosa, watu walikuwa wanaona kawaida tu mtu kulazimisha mapenzi au mahusiano. Watu wengine hadi leo wanaombana msamahana kwa masale baada ya kubaka, hawajui ni kosa la jinai.
Tulielimishana kama TAPO, TGNP ilitusaidia kuelewa hekaya (narratives) TGNP ilisaidia sana kama Mtandao kuelewa zile hekaya zilizozeeka.
Wakati huo, tulijitahidi sana, kujenga nguvu ya vyombo vya habari, ili wawe sehemu ya Tapo, tukawaelimisha wanahabari wakaielewa ajenda na kuhakikisha wanasaidia kutoa elimu. Tukawa wana wanasheria ambao walikuwa waanaandika vitu kwa lugha rahisi ili watu waelewe, tulitumia waalimu, madaktari wa Muhimbili baadhi waliungana na sisi kuelea na kutafisiri kwa lugha rahisi madhara ya kuingiliana kimwili kwa lazima bila ridhaa ilisaidia sana dhana ya Ukatili wa ubakaji kueleweka.
Tulijenga maudhui yanayoelimisha watu binafsi, tulielimusha watu wajue kwamba suala la ubakaji sio swala la kawaida, na sio la kuchekelea, na tulihakikisha wanaume wanaielewa hiyo dhana na wanakuwa chanzo cha mabadiliko. Tuliengeneza mahudhui yaliyosambazwa kwa vyombo vya habari, yaliyowagusa watu wote ili kila mtu aone kwamba ni muhimu kuwa na sheria hiyo.
Jambo lingine ni kwamba harakati hizi zilikuwa endelevu, hatukupoa, “ hakuna wakati katika historia ya ufeminia Tanzania, ambapo wanaharakati walijitoa kwa hali na mali na rasilimali zao, muda na fedha bila kupoa. Tulikesha usiku na mchana kuandika press release, watu walienda Dodoma kwa gharama zao, walilala kwenye mahema, hakukuwa na fedha za wafadhaili, tulisimama kwa uchungu, tulihakikisha Tunadai mabadiliko ya haraka.
Mikakati yetu ni kuelewa muktadha, na tulitumia mbinu makini sana, miaka ile 1990, ndio Ukimwi ulikuwa umeshamiri kwa kasi kubwa. Tulihusisha ubakaji na maambukizi ya HIV na tukahusisha muktadha wa wakati ule na HIV ili watu wakubali sheria ipite . tukaeleza UKIMWI na Ubakaji na madhara yake. Wafeminia katika miaka ya 1999, walikuwa wakijitoa, bila ubaguzi,kujibakiza, tulijitoa kwa nguvu kubwa sana. Walikusanya ushahdii wa kina ili sherikali iandae muswada, lakini pia TGNP ilituunganisha kuwa na marafiki wengi walio serikalini,
Nguvu ya pamoja na sauti ya pamoja, kuna wakati ulikuwa huwezi kuona shirika moja limesimama, tulikwdna pamoja kama wafeminia wamoja, na agenda tuliibeba kwa pamoja, na ilipata suluhu ya haraka.
Watu walikuwa na udhubutu, Eda sanga alikuwa radio Tanzania, ni chombo cha erikali, lkni alikuwa na udhubutu, akasimama Bungeni kwa ujasiri mkubwa akawaeleza wabunge kwamba, “sisi wanaharakati tutasimama kwa pamoja kuhakikisha, Mbunge yeoete, ambaye hataipigania sheria ya SOSPA tutasimama kwenye jimbo lake kuwataka wananchi wote hasa wanawake wasimpe kura” Huu ulikuwa ujasiri wa hali ya Juu.
Social Plugin