TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)mkoa wa Shinyanga, imebaini kiasi cha Tshs million 83.3 za kodi ya zuio kutowasilishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka wa wazabuni na watoa Huduma katika mkoa wa Shinyanga na Kufanya serikali kupoteza mapato.
Akisoma
taarifa ya uchunguzi huo kwa vyombo vya habari mapema leo Septemba 06, 2023
katika ofisi za TAKUKURU Mkoani Shinyanga.
Kaimu
mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani humo Mwamba
Masanja amesema uchambuzi huo ulibaini kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jumla
ya Sh. 83,328,256.81 fedha za kodi ya zuio zilizokatwa kutoka kwa wazabuni na
watoa huduma hazikuwasilishwa kwa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato Tanzania TRA.
“Tumebaini kuwa zaidi ya milioni 83 fedha za fedha
za kodi ya zuio zilizokatwa kutoka kwa wazabuni na watoa huduma
hazikuwasilishwa kwa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato Tanzania TRA kama sheria inavyoelekeza,
sababu zilizopelekea kutowasilishwa kwa fedha hizo ni pamoja na mabadiliko ya
mfumo wa TRA (Tax Payer Portal), uelewa mdogo juu ya mapato hayo pamoja na
wazabuni na watoa huduma kutokudai stakabadhi za makato ya kodi ya zuio
waliyokatwa”, alisema Mwamba Masanja.
Aidha Masanja
amesema TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi hicho yenye thamani ya shilingi
Bilioni 16.2 na kubaini dosari ndogondogo kwenye miradi ya sekta ya elimu,
afya, maji na ujenzi.
“Mradi wa ujenzi wa kituo cha
afya bulige haujakamilika na ujenzi wa shule ya msingi maganzo umebainika kuwa
jengo la utawala halijawekwa vigae, roof board haina ubora, vyoo vya wavulana
kukukosa ventilation, madarasa ya chekechea mikanda ya gypsum boadi imeanza
kubanduka na bembea upande wa chekechea hazijawekwa”, alisema Masanja.