Na Mathius Canal, Dodoma.
Ujumbe wa Marafiki waliosoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Mb) ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe umetoa pongezi kwa Dkt. Biteko kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Wametoa pongezi hizo leo Novemba 3, 2023 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma ikiwa ni pamoja na kumtakia heri katika majukumu yake mapya ambapo wamesisitiza kuunga mkono juhudi za Serikali.
Kwa upande wake, Dkt. Biteko amewashukuru kwa kumtakia heri na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili azma ya Mhe. Rais Samia itimie katika kujenga uchumi wa nchi na Watanzania wanufaike.
Ujumbe huo ni wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza (SAUT) na marafiki wengine waliosoma maeneo mbalimbali nchini.
Social Plugin