Picha ya pamoja kati ya wakulima na Mwakilishi Mkuu wa JICA, Ara Hitoshi wakati wa ziara katika miradi inayotekelezwa nao Mkoani Kilimanjaro.
Mkulima na Mnufaika wa mradi huo, Selina Minja akitoa ushuhuda wake juu ya manufaa ya TANSHEP katika kilimo alichofanya.
Mwakilishi Mkuu wa JICA, Ara Hitoshi akizungumza na wakulima walionufaika na mradi TANSHEP, Wakati Wa ziara ya wana habari Mkoani Kilimanjaro.
Wakulima na wanufaika wa mradi TANSHEP wakiwa wanamsikiliza Mwakilishi Mkuu wa JICA, Ara Hitoshi wakati ziara ya maeneo yao ya kilimo.
Mwakilishi Mkuu wa JICA, Ara Hitoshi akikabidhiwa zawadi na wanufaika Wa mradi Wa tanshep kwa mkoa Wa Kilimanjaro ikiwa kama shukrani yao.
(PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY)
****
Na James Salvatory
Wakulima nchini wametakiwa kujikita kwenye kilimo biashara kwa kubadilisha mfumo wa kulima na kuuza mazao yao na badala yake kutafuta masoko kabla ya kuanza kulima ili kupata faida na tija kwenye kilimo chao.
Wito huo umetolewa na Afisa kilimo na mratibu wa mradi wa kuimarisha mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya na uwezekaji kwa kutumia mbinu ya SHEP(TANSHEP) kwa halmashauri ya wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Hamza Mwinyihija katika ziara ya wanahabari ya kuembelea miradi inayotekelezwa katika mkoa huo
na Arusha.
Mwinyihaji amesema kupitia TANSHEP kilimo biashara kimekuwa msaada kwa wakulima wengi kufahamu Hali ya soko na namna ya kulima kulingana na uhitaji husika.
Amesema wao kama halmashauri wameweza kunufaika kupitia mradi huo kwa wakulima wengi zaidi kujifunza mbinu mpya za kilimo kutoka mbinu ya kizamani ya kuzalisha na kuanza kuuza na kuzalisha ili uuze.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Ara Hitoshi amesema kuwa kutokana na mradi huo zaidi ya wakulima 3,000 katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga wamenufaika na mradi huo na mapato ya vikundi maalumu yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 25.
Awali akinguzungumza mkulima na Mnufaika wa mradi huo, Selina Minja amesema hapo awali walikuwa wanalima kwa mazoea ila toka TANSHEP iwafikie imekuwa na manufaa makubwa kwa sababu wanachokilima kinakuwa kimeshanunulia hivyo kuepukana na hasara za mazao yao kutokupata soko.
Aidha ameishukuru JICA kwa kuwanufaisha kwa ujio wa mradi huo na kuwaomba kuwafikia wakulima wengine nchini.
Social Plugin