Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoania Shinyanga Bw. Joseph Mkude akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) Novemba 14,2023, katika viwanja vya shule ya Msingi Idukilo, kata ya Idukilo mafunzo yaliyojumisha wahitimu 224 wanawake 17 na wanaume 207
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson akizungumza kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) love Novemba 14,2023 katika viwanja vya shule ya Msingi Idukilo, kata ya Idukilo.
***************
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bw. Joseph Mkude amefunga mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) tarehe 14/11/2023, katika viwanja vya shule ya Msingi Idukilo, kata ya Idukilo mafunzo yaliyojumisha wahitimu 224 wanawake 17 na wanaume 207
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo Mkuu huyo ametoa pongezi na shukrani kwa viongozi wa kata ya Idukilo kwa kuhakikisha mafunzo ya jeshi la akiba "Mgambo" yameanza na kumalizika salama, huku akiwashukuru Wakufunzi waliohusika kutoa mafunzo na kuwafanya wanafunzi kuhitimu mafunzo hayo kwa viwango vinavyohitajika.
" Ninawapongeza na kuwashukuru sana wakufunzi wote mliotoa mafunzo haya ya viwango vinavyohitajika, wahitimu wote mkawe mstari wa mbele katika kuilinda, nchi yenu na kuwa mstari wa mbele kujitolea kazi mbalimbali za ujenzi wa Taifa,
Vilevile mafunzo mliyoyapata yakawe ni sehemu ya kupeleka elimu kwa jamii juu ya maadili mema, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na usalama katika kutoa taarifa za uhalifu popote pale unapotokea." Alisema Mkude
Aidha Mkude ametoa wito kwa makampuni yote ya ulinzi wilayani kuajiri vijana waliopitia katika mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) na kuwapa kipaumbele katika nafasi za Jeshinla Kujenga Taifa ( JKT ).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson amewapogeza sana wahitimu pamoja na wakufunzi kwa kumaliza salama mafunzo pamoja na kuahidi kutenga bajeti kupitia Mapato ya ndani kwaajili ya sare za Jeshi la akiba
Naye Mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Kishapu (OCD) Esther Gesogwe amewataka wahitimu wote kuhakikisha usalama maeneo yote ambayo watakuwepo na kushirikiana kwa ukaribu na Jeshi la Polisi pamoja na kuimarisha Amani.
Aidha mafunzo hayo yalianza Julai 10, 2023 na kumalizika Novemba 15 ,2023 yenye lengo la kuwajengea uwezo vijana hao ili kuimarisha ulinzi na usalama ndani na nje ya Wilaya hiyo.
Social Plugin