Kikundi cha Nguvu Moja kilichopo manispa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga kimeshauriwa kuja na mipango madhubuti ya uanzishaji wa miradi itakayosaidia jamii pamoja na wanachama wa kikundi hicho.
Ameyasema hayo jana Novemba 18,2023 afisa maendeleo ya jamii
mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale wakati akizungumza na wanachama wa kikundi cha
Nguvu Moja kwenye hafla ya kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Amesema ni wakati sasa wa vikundi na wanachama kufikiri kwa
mapana zaidi namna ya uanzishaji wa miradi kwenye vikundi vya kusaidiana, itakayowasaidia
wanachama na jamii kwa ujumla.
“Tusiishie tu kusaidiana kwenye shida na raha bali tuangalie namna gani tunaweza kuisaidia jamii, na kuwa mfano kwa vikundi vingine, vikundi vingi vinavyoanzishwa vinashindwa kuendelea kutokana na kushindwa kubuni na kusimamia miradi itakayowainua wanachama, mbali na kusaidiana katika shida na raha, tuangalie pia namna gani tunaweza kuisaidia jamii kupitia vikundi tunavyovianzisha",
"Kupitia fursa
zilizopo ndani ya mkoa huu, twendeni tukazalishe kwa ukubwa ili tuweze kuleta
manufaa kwa wanakikundi na jamii inayowazunguka, na hatimaye malengo ya kiukundi
hiki yakaonekane ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga, macho hayana thamani ikiwa mawazo
yetu yamefungwa”, aliongeza Tedson Ngwale.
Akisoma risala kwa
mgeni rasmi Velma Moris ameeleza malengo ya kikundi hicho ikiwa ni pamoja na
kusaidiana baina ya wanachama katika shida na raha sambamba na kutoa mafunzo ya
biashara na ujasiriamali ili kutengeneza jamii yenye kusimamia uchapaji kazi.
“Kikundi hiki kilianzishwa tarehe 20/11/2022 kikiwa na
wanachama 20 kwa lengo la kukuleta umoja
baina ya wanachama ili kusaidiana katika shida na raha ambapo kwa sasa
kina wanachama 53, ambapo 45 ni wanawake na 8 ni wanaume, tumejipanga kuanzisha
miradi mbalimbali itakayoweza kuendesha kikundi chetu, lakini pia tumedhamiria
kwa siku zijazo kutoa mafunzo kwa wanachama juu ya ujasiriamali na biashara kwa
wnanchama ili kusaidia wanachama kupata ujuzi wa kukuza na kuendesha biashara,
lakini pia kuwa mabalozi wa kupinga vitendo vya ukatili,” alisema Velma Moris.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi , afisa tarafa ya Samuye
Aaron Laizer amekipongeza kikundi hicho kwa kutoa kipaumbele kwa
wanawake huku akimuomba afisa maendeleo
mkoa kutoa elimu kwa wanachama na vikundi mbalimbali ili kuwajengea uwezo.
“Niwapongeze
sana kwa idadi kubwa ya wanawake kwenye kikundi hiki cha nguvu moja hii ni wazi kuwa mmetambua nafasi ya mwanamke kwa kutoa kipaumbele, pia
kwa hotuba hii kutoka kwa mgeni rasmi nilitamani ikawe mafunzo kwa wananchama
na vikundi mbalimbali kuwajengea uwezo waweze kuwa na mawazo nyenye kuleta
mafanikio makubwa”, Alisema Aaron Laizer.
Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza na wanachama wa kikundi cha Nguvu Moja.
Velma Moris akisoma risala ya kikundi cha Nguvu Moja wakati wa hafla hiyo.
Afisa tarafa ya Samuye Aaron Laizer akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi wakati wa Hafla hiyo.
Wanachama wa kikundi cha Nguvu Moja.
Mwenyekiti wa kikundi cha Nguvu Moja Leopodin Masai akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Katibu wa kikundi cha Nguvu Moja Kosta Kasisi Akizungumza wakati wa hafla hiyo.
<<<<PICHA MBALIMBALI>>>>
Social Plugin