Mwenyekiti wa Mtaa wa Chikoha, Kata ya Bihawana Paulo Mtwe akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea eneo hilo November 2,2023.
Na Dotto Kwilasa, Dodoma.
ZAIDI ya Wananchi 300 wa Mtaa wa Chikoha kata ya Bihawana,jijini hapa wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi katika maeneo yao ambayo wanadaiwa kuvamia .
Mmoja wa wanananchi na mmiliki wa sehemu ya eneo hilo Isack Mjelwa amewaambia waandishi wa habari kuwa wamekuwa wamiliki wa maeneo hayo toka enzi za mababau lakini cha kushangaza wanaitwa wavamizi wa maeleneo yao.
Amesema tangu shughuli za Serikali kuhamia Dodona,kero na migogoro ya ardhi ya hapa na pale imekuwa haiishi na kupelekea watu wa hali ya chini kuporwa ardhi yao bila utaratibu.
"Kila kukicha wanakuja watu mbalimbali kwa ajili ya kuja kututisha wanasema maeneo ni ya Serikali sasa tunashindwa kuelewa serikali imepata maeneo haya kwa nani na sisi tunamiliki maeneo haya toka enzi za mababu, " anasema na kuongeza;
"Ukija kuangalia kwenye maeneo haya kuna makaburi ya babu zetu wa enzi na enzi hawa ndugu zetu walizikwa hapa na juzi hapa wamekuja watu kwajili ya kuweka mabango na wamekuja na maaskari na mitutu kututishia kuhusu maeneo yetu wanasema kuna viongozi ngazi ya Wilaya ndiyo waliwatuma kwajili ya kulitwaa hili eneo na kama eneo ni mali yao wanashindwaje kuja kukaa na sisi?alihoji
Njelwa amesema,"kwa kuwa tunaelewa Dodoma sasa ni jiji tunapaswa kuendana na mabadiliko lakini mabadiliko hayo yasiwe chanzo cha dhuluma na unyanyasaji kwetu,
Tunahitaji kukaa na kukubaliana,tunaomba tupimiwe maeneo yetu lakini siyi wa vitisho ,kwasababu Serikali yetu ni sikuvu tunaiomba itusaidie kwa haya maeneo yetu tunanyanyaswa mno hata ulimaji wetu unakuwa mdogo ,"amesema Mjelwa.
Kwa upande wake Maria Zakaria ameeleza kuwa
"Sisi ni wazaliwa wa hapa wala siyo wageni ni maeneo yetu wala siyo ya serikali,tunanyanyaswa kila kukicha tunaomba suluhu ya hili tatizo.
"Wasomi wanatunyanyasa sana wanatuibia sisi ambao hatuelewi kitu chochote kama mimi nitaenda wapi,hata pa kuanzia sielewi,haya maeneo mnayoana hapa ni yetu na sisi ndio wamiliki halali tunaomba serikali itufikirie,tutapeleka wapi familia zetu jamani,twende tukafie wapi wanatumaliza,"amesema
Kwa upande wake Stivin Matereka alieleza kuwa yeye ni mzaliwa wa eneo hilo tangu miaka mingi wanahama vijiji vya ujamaa,wengine na kufafanua kuwa baadhi ya ndugu zao walihamia Mbabala, Michese na Mkonze lakini huku baadhi ya shughuli zao ikiweni kilimo walikuiwa wanazifanya katika maeneo hayo ya Chikowa.
"Tuliishi vijiji vya ujamaa tukazaliana ardhi ikawa ndogo tukaanza kurudi kulima tulipotoka ambapo ni hapa, tunashangaa kuna mtu anaibuka kusema maeneo haya ni yake na kudai kama ni yetu basi tuoneshe umiliki halali,hizo hati tunazitoa wapi wakati tumerithi kimila, " Anafafanua.
Kutokana na hayo Mwenyekiti wa Mtaa huo,Paulo Mtwe ameeleza kuwa kuna malalamiko kuhusu hilo eneo,lakini toka awali wananchi walikuwa wanayamiliki maeneo hayo kabla ya ujamaa na baada ya ujamaa ambapo Mwalimu Nyerere aliwakusanya kwenye sehemu moja na kuwa na vijiji vya pamoja na kujitegemea lakini baada ya hivyo vijiji waliendelea kuyamiliki maeneo hayo kwa kilimo , ufugaji na kamazi.
"Tuliishi kwa amani lakini sasa kila kukicha wanakuja wageni kudai hili eneo kuwa ni lao jambo ambalo sio kweli,huu umekuwa uonevu ambao Serikali inapaswa kuukataa, hivi karibuni niliitwa mimi kama Mwenyekiti kwenye ofisi ya mkuu wa Wilaya nilivyoenda ilikuwa siku ya ijumaa kwa kweli nilipewa vitisho vikali mno niliingia ile ofisi saa tano ya asubuhi niliruhusiwa saa 12 jioni naambiwa kuwa wewe Mwenyekiti ndiyo tatizo wanachi hawana shida tatizo ni wewe Mwenyekiti ndiyo unayeshawishi wawe wakali,"amesema
Naye mtaalam wa ardhi kutoka jiji la Dodoma ,Enock Katete akiwa ni mmoja kutoka kwenye kamati au timu iliyoiagizwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini kufuatilia suala la eneo hilo alisema kwa mujibu wa kumbukumbu na taarifa ambazo kikosi kazi kilipitia ni kwamba eneo hilo ni miongoni mwa maeneo ambayo yalitengwa kwa ajili ya ukanda wa kijani na Mamlaka ya ustawishaji makao makuu (CDA ).
Amesema kumbukumbu zinaonesha eneo hilo lilitokana na oparesheni ya vijiji la mwaka 1972 hadi 1974 na waliyokuwepo kwenye maeneo hayo waliamishwa kwenda kwenye maeneo mengine kwahiyo eneo likabaki kwa matumizi ya ukanda wa kijani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri alitoa siku 30 kwa wakazi wa eneo hilo kuhakikisha wanasimanisha shughuli zozote kwenye eneo hilo na kwamba kwa atakaye kiuka agizo hiilo au kuwekeza kitu chochote atachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu eneo hilo linaumiliki wa vyombo vya usalama .
Pamoja na hayo amewataarifu wananchi hao kuwa ikiwa wana uhitaji wa ardhi wajiorodheshe majina yao ili Serikali ione nanma ya kuwasaidia katika maeneo mengine ambayo jiji wanapima na kupanga mji waweze kumilikishwa kwani hayo ndiyo maelekezo ya Serikali .
Social Plugin