Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TABORA,MARA WAANZA UBORESHAJI WA MAJARIBIO WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


Uboreshaji wa Majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura umeanza leo Novemba 24,2023 katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya na Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.


Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe. Mwanaisha Kwariko ametembelea vituo vya kuandikisha wapiga kura katika Kata ya Ikoma na kushuhudia wananchi wa kata hiyo wakijitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao.


Akizungumza baada ya kutembelea vituo hivyo, Mhe. Mwanaisha amesema wananchi wa Kata ya Ikoma wamejitokeza mapema kwenye vituo na uboreshaji unafanyika kwa amani na utulivu.


Hivyo ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Ikoma ambao wana sifa za kujiandikisha na wale wanaotaka kuboresha taarifa zao wajitokeze kwa wingi ili kuboresha taarifa zao.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akizungumza na wananchi na wapiga kura waliojitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Kituo cha Kuandikishia Wapiga Kura cha Shule ya Sekondari Kazehill iliyopo Kata ya Ng'ambo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora.


"Tume inafanya majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye kata hiyo kuanzia leo tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023. Uboreshaji huo unafanyika pia katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, mkoani Mara",amesema.


Mkurugenzi wa Uchaguzi ametembelea vituo vyote 10 vya kuandikishia wapiga kura kwenye kata hiyo. Zoezi hilo linaendelea vizuri ambapo vituo vimefunguliwa saa 2:00 asubuhi na vitafungwa saa 12:00 jioni.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com