WILAYA YA KONGWA KUTANGAZA UTALII WAKE KUPITIA MICHEZO

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Remidius Mwema akizungumza na waandishi wa habari Dodoma kuhusu kuanza kwa mbio za Marathon kwa lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji,utalii na historia ya Wilaya hiyo. 


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini imeandaa mbio za Marathon kwa lengo la kuutangaza mchango wa Wilaya hiyo na Tanzania kwa ujumla katika ukombozi wa nchi za Afrika. 

Kupitia mbio hizo Ofisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuyatambua maeneo ya kihistoria, kuyalinda, na kuyaendeleza ili kuenzi historia yataifa na kuyafanya sehemu ya utalii wa kihistoria katika maeneo ya urithi wa ukombozi yaliyopo nchini.

Hayo yameelezwa leo November 16,2023 Jijini hapa na Mkuu wa Wilaya hiyo Remidius Mwema wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya kuitangaza wilaya hiyo kupitia mbio za marathon zitakazoanza November 25,2023 wilayani Kongwa mkoani hapa. 

Amesema mbio hizo  ambazo zimepewa jina la "Kongwa liberation Marathon"imezingatia taratibu zote za marathon na kwamba zimegawanywa kwenye makundi ya Kilomita 5,Kilomita 10 na Kilometa 21 huku mgeni rasmi wa mbio hizo akitarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro. 

Amesema Wilaya ya Kongwa imegusa ukombozi na historia ya harakati za ukombozi wa nchi za  kusini mwa Afrika zikiwemo Afrika ya Kusini,Zimbabwe,Angola na Msumbiji na hivyo kuwa na nafasi ya kujitangaza kama sehemu ya vivutio vya utalii. 

"Serikali itashirikiana na nchi tulizozipa hifadhi wakati wa harakati za ukombozi kwa kukarabati majengo yaliyotumika na wapigania uhuru wa Afrika ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wao na kuitunza historia hiyo kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae” amesema 

Amesema kupitia Marathon Wilaya hiyo itatangaza fursa za Uwekezaji zilizopo ikiwemo  Kilimo,Viwanda,Ranchi ya taifa,Soko la kimataifa la mahindi Kibaigwa na Hoteli za kitalii . 

"Kwa kuwa Kongwa ni lango la kuingia makao makuu ya nchi tunategemea kuwa sehemu ya kivutio cha utalii na uhifadhi wa historia,hivyo tumetenga eneo la Pandambili kwa ajili ya Uwekezaji wa Viwanda,tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza, " Amesema na kuobgeza;

"Niwaombe wana Dodona na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu
kuendelea kutangaza fursa zetu
kama ambavyo Serikali yetu ambavyo imekuwa ikijitolea  fedha kukarabati baadhi ya maeneo muhimu ya kihistoria kupitia wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo, "amesema



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post