Waumini na Watumishi wa Mungu wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuliombea taifa na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita kwa niaba ya Naibu waziri mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Waadventista wa Sabato Nyahanga Ukanda wa Dhahabu, ambapo amesema, ni wajibu kumuombea Rais na Taifa ili kuilinda amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo.
Mhita amesema, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kwaajili ya kuleta maendeleo ya taifa hivyo ni wajibu wa waaumini na watumishi wa Mungu kumuombea ili awe na nguvu na mshikamano katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Katika Ibada hiyo Naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati amekabidhi kiasi cha Shilingi milioni 10 kama mchango wa ujenzi wa kanisa hilo, huku Mbunge wa Ushetu Emanuel Cherehani akitoa shilingi milioni 1.
Katika hatua nyingine Askofu wa jimbo la Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo amemshukuru Naibu Waziri mkuu kwa majitoleo yake katika kufanikisha ujenzi huo ambapo mahitaji ya ujenzi ni shilingi Milioni 250.
Mwakilishi wa katibu wa mbunge wa jimbo la Ushetu Bwana Philipo Chimi Fundi akifuatilia ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Waadventista wasabato Nyahanga Ukanda wa Dhahabu.
Baadhi ya waumini wa kanisa la Waadventista wasabato Nyahanga Ukanda wa Dhahabu, waliohudhuria katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin