Na. Gideon Gregory-DODOMA
MABINGWA Watetezi Yanga SC wameibuka na ushindi ugenini baada ya kuichapa bao 1-0 Timu ya Tabora United mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Bao la ushindi la Yanga SC limefungwa na Kiungo Mshambuliaji Stephane Aziz Ki dakika ya 21 kwa Mpira wa faulo uliomshinda mlinda mlango wa Tabora United.
Bao la Aziz ki limekuwa la 10 msimu huu na kuwaacha nyuma Mshambuliaji wa Simba Jean Baleke na kiungo Mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum wenye mabao 8.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha Pointi 30 ikiwa nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 11 huku Azam FC wanaendelea kukaa kileleni wakiwa na pointi 31 wakicheza mechi 13,nafasi ya tatu inashikwa na Simba SC wenye Pointi 23 wakiwa wamecheza mechi 10.
Social Plugin