MJUMBE wa Baraza Kuu la Wazazi na Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mkoani Mwanza Velji AminMohamed amezitaka Jumuiya ya Wazazi Mkoani hapo kubuni Miradi ya uzalishaji mali waweze kujiendesha vizuri.
AminMohamed Maarufu kama "Mlete Mzungu" ameyasema leo katika Kata ya Igoma Jijini Mwanza kwenye tukio lililofanywa na Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Igoma kugawa pampasi na sabuni kwa kina mama waliojifungua kwenye Kituo Cha Afya kwenye eneo hilo.
"Ndugu zangu umoja ni Nguvu hivyo imarisheni Mshikamano Ili muweze kupata Ukombozi wa kiuchumi kwani Uchungu wa Mwana aujua Mzazi" alisema Mohamed.
Alisema kuna umuhimu kwa Jumuiya ya Wazazi kuwa na Miradi ya uzalishaji mali Ili waweze kujiendesha wenyewe kwani uwezo wa kiuchumi ni mhimu kwa usitawi wa Taifa.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Igoma Jesca Nzungu alipongeza ziara iliyofanywa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa kutoka mkoani hapo kwa kuwaunga mkono kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Aliwataka wazazi katika Kata hiyo kuwa karibu na watoto wao katika kipindi Cha likizo Ili kuwajenga kimaadili waweze kuwa watu wema Kwa usitawi wa Taifa la Tanzania.
Social Plugin