Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROFESA NDALICHAKO AIPONGEZA GGML UDHAMINI TUZO MUAJIRI BORA 2023

 
Makamu Rais wa AngloGold Ashanti -GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ubia/ ushirika (Afrika), Simon Shayo akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa muajiri bora wa mwaka 2023 - zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) hivi karibuni jijini Dar es salaam. Shayo alisema GGML ambayo ilikuwa mmoja wa wafadhili wa hafla hiyo, zaidi ya asilimia 80 ya menejimenti ya kampuni hiyo inaongozwa na Watanzania hivyo kuwa mgodi kinara unaoajiri Watanzania wengi tofauti na kampuni nyingine za sekta ya madini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako akimpatia cheti cha shukrani Meneja Mwandamizi wa Rasilimali Watu kutoka GGML, Charles Masubi baada ya kampuni hiyo kuwa mmoja wa wadhamini wakuu wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa muajiri bora wa mwaka 2023 - tuzo ziliandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano, Stephen Mhando akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bwana Oscar Mgaya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na menejimenti ya GGML katika hafla hiyo ya ugawaji wa tuzo za muajiri bora kwa mwaka 2023.
Baadhi ya wafanyakazi wa GGML wakifurahia cheti cha shukrani walichokabidhiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo kwa mwajiri bora kwa mwaka 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com