JAMII YAASWA KULINDA WATOTO WA KIUME DHIDI YA NDOA ZA JINSIA MOJA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Aliko Mbuba

Na Mwandishi wetu, Mbeya

Jamii imeaswa kuongeza nguvu katika kutetea haki za watoto wa kiume ili kuwaepusha na ndoa za jinsia moja jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Wito huo umetolewa Desemba 29,2023 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Aliko Mbuba wakati akifungua kikao kazi cha kupokea mrejesho wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia kilichoandaliwa na TGNP.


“Wakati mwingine tunagundua kwamba haki za wasichana na wanawake zinavunjwa na kusahau kuwa haki za watoto wa kiume, vijana na wanaume nazo zinavunjwa. Ni lazima tuchukue hatua kutetea haki za jinsi zote, me na ke. Wengi wamekuwa wakitilia mkazo haki za wasichana na wanawake tu. Kufanya hivyo kumepelekea baadhi ya watoto wa kiume kuolewa,” alisema bwana Mbuba.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Aliko Mbuba.

Alionya kuwa sheria za nchi haziruhusu ndoa za jinsia moja na kukumbusha kuwa ni vema jamii ikaongeza nguvu kuwalinda watoto wa kiume ili wasitamani kuwa wanawake.

Katika kikao hicho, Wawakilishi kutoka vituo vya taarifa na maarifa walifanya mawasilisho ya tathmini ya bajeti katika sekta za afya, elimu, kilimo, maji na ujengaji uwezo kwenye masuala ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa Mshauri mwelekezi kutoka TGNP Bi. Rose Ngunangwa, mafanikio ya utekelezaji wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia katika wilaya ya Mbeya ni makubwa kuliko changamoto kwani wamefanikiwa kujenga vituo vingi vya afya ambavyo vinatoa huduma kwa mama na mtoto.
Mshauri mwelekezi kutoka TGNP Bi. Rose Ngunangwa.

Vilevile, vijiji vingi katika wilaya hiyo vimeunganishwa na maji safi na salama huku miradi mipya ya maji ikiwa mbioni kutekelezwa.


Kwa upande wa elimu, shule zote zina huduma ya vyoo, maji na vyumba vya usiri ambapo huduma za taulo za kike zinatolewa katika shule zote za sekondari wilayani humo.

Miongoni mwa changamoto zilizoainishwa katika kikao kazi ni kufutwa kwa bima ya mama na mtoto na kusitishwa kwa mikopo ya asilimia 10 katika halmashauri ambapo serikali imeombwa kurudisha huduma hizo.

Changamoto nyingine ni upungufu wa wataalamu wa afya katika vituo vya afya.

Akijibu kuhusu changamoto hizo, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bi. Mary Mwakyembe alikiri kuwa upungufu wa watalaamu wa afya ni tatizo la nchi nzima hata hivyo wamekuwa wakijitahidi kuongeza pale wanapopata fursa ya kufanya hivyo.

Kuhusu bima, Bi. Mwakyembe aliwashauri wananchi kujiunga na bima ya afya kwa wote ili kukabiliana na adha ya gharama za matibabu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Aliko Mbuba akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha mrejesho wa uchambuzi wa Bajeti kilichoandaliwa na TGNP
Afisa kutoka TGNP, Vera Assenga akizungumza wakati wa kikao kazi cha mrejesho wa uchambuzi wa Bajeti kilichoandaliwa na TGNP
Afisa kutoka TGNP, Vera Assenga akizungumza wakati wa kikao kazi cha mrejesho wa uchambuzi wa Bajeti kilichoandaliwa na TGNP
Mshauri mwelekezi kutoka TGNP Bi. Rose Ngunangwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha mrejesho wa uchambuzi wa Bajeti kilichoandaliwa na TGNP
Mshauri mwelekezi kutoka TGNP Bi. Rose Ngunangwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha mrejesho wa uchambuzi wa Bajeti kilichoandaliwa na TGNP
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Wazidi Mahenge akizungumza wakati wa kikao kazi cha mrejesho wa uchambuzi wa Bajeti kilichoandaliwa na TGNP
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Wazidi Mahenge akizungumza wakati wa kikao kazi cha mrejesho wa uchambuzi wa Bajeti kilichoandaliwa na TGNP


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post