Na.Bolgas Odilo-Mzalendo blog
SIMBA SC imeweka Matumaini ya kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuichapa mabao 2_0 Wydad Casablanca mchezo wa kundi B uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na Willy Onana dakika ya 36 na 38 hadi mapumziko Simba walienda wakiwa kifua mbele.
Kwa matokeo hayo Simba SC wamefikisha jumla ya na pointi tano na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi ikisaliwa na michezo miwili dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast ugenini Februari 23,2024 na Jwaneng Galaxy ya Botswana Machi 1,2024.
ASEC Mimosas akiwa anaongoza msimamo akiwa na Pointi saba atashuka uwanjani kucheza na Jwaneng Galaxy ya Botswana.
Social Plugin