Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa akiwa kwenye picha ya pamoja katika ufunguzi wa mafunzo maalumu ya ubunifu na ujasiriamali yaliyoandaliwa na shirika la maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa akizungumza akizungumza Kando ya mafunzo maalumu ya ubunifu na ujasiriamali yaliyoandaliwa na shirika la maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Ara Hitoshi akizungumza na waandishi wa habari
Afisa utawala na Mawasiliano JICA Tanzania, Alfred Zacharia, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo maalumu ya ubunifu na ujasiriamali
Washiriki Mbalimbali wa mafunzo maalumu ya ubunifu na ujasiriamali wakizungumza kwa nyakati tofauti.
**************
Na MWANDISHI WETU
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa amesema kuna umuhimu wa wanafunzi wa Tanzania kupatiwa elimu ya ubunifu na ujasiliamali ili kuwawezesha kujiendeleza kiuchumi watakapokuwa chuo na hata watakapokuwa wamemaliza masomo yao .
Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo maalumu ya ubunifu na ujasiriamali yaliyoandaliwa na shirika la maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
"Sisi kama ubalozi wa Japani tuliona kwamba ni muhimu wanafunzi hawa wakapata elimu ya moja kwa moja kutoka kwa wataalam wa biashara na ubunifu," alisema Misawa.
Misawa alisema matumaini yake wanafunzi hao watatumia mafunzo hayo katika kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri wenyewe na hata wakiajiliwa kuweza kufanya kazi kwa ueledi na ubunifu wa hali ya juu.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye alisema lengo la mafunzo hayo ni kuunganisha nadharia na vitendo kwenye masomo ya ubunifu.
"Hii ni fursa kwa Watanzania hasa kwa wanafunzi wa chuo cha Dar es salaam kujifunza masuala ya ubunifu kutoka kwa wataalam wa ubunifu wa Japani na Kuna wakufunzi wa chuo hichi ambao ni wataalam wa masuala ya kukuza ubunifu na ujasiliamali," alisema Profesa Anangisye
Pia alisema mafunzo hayo yatawawezesha wanafunzi hao kujiajiri na kuajili watu wengine pindi watakapo maliza chuo na hata kuendelea na biashara za ujasiliamali wakati wakisubiri kuajiliwa.
Anangisye alisema katika Chuo chao wamefanikiwa kuweka misingi imara ya kuhakikisha wanafunzi wao wanafanikiwa ndio maana wameamua kuwashirikisha wabunifu kutoka japani kwasababu Japana wapo mbali sana kwenye ubunifu na ujasiliamali.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa UDSM, Zulpha Mkumba alisema wanafunzi wengi wanaelimu ya biashara na mawazo ya kufanya biashara lakini wanakosa mafunzo ya kujifunza jinsi gani watafanyabiashara zao kwa ubunifu na kuendenda sawa na soko la wakati huo.
"Kupitia mafunzo haya naamini kila mwanafunzi hataongeza ujunzi wa biashara kwasababu wafanyabiashara wengi hasa waliotoka shule huwa wanaelimu nzuri ya biashara lakini alianzisha biashara yake Kuna kipindi anaweza kukwama kwasababu halikosa mafunzo kama haya," alisema Mkumba.
Aliushukuru uongozi wa chuo hichi na WA Jaica kwa kuwapatia mafunzo ambayo yanakuwa kama mwongozo wa wao pindi watakapoanza kufanya biashara zao kabla ya kurudi mtaani.
Naye Mwanafunzi wa fani ya Kilimo,Biashara, Maliasili na Uchumi wa UDSM, Hassan Nyamanga mafunzo hayo yataenda kuwasaidia kuendeleza mawazo yao ya biashara na kufanya biashara zao kulingana na ushindani wa soko lililopo.
"Mafunzo haya yatasaidia kumjenga mwanafunzi kufikiria kuhusu masuala ya ubunifu katika kuendeleza biashara yake hata hasipoajiriwa serikali au kwenye taasisi binafsi bado hatakuwa anauwezo wa kuendesha biashara zake binafsi kwa kuendenda sawa na soko la Dunia," alisema
Aidha aliiomba serikali kuwawekea mitaala ya kujifunza kwa vitendo kama mafunzo wanayopatiwa Sasa na Japani ili kumjenga wanafunzi pindi hatakapohitimu masomo yake.
Mwisho.
Social Plugin