Na Pamela Chaula Tanga
Katibu wa Halmashauri kuu ya Oganaizesheni ya CCM Taifa Issa Haji Gavu amewasili mkoani Tanga na kuzungumza na mabaraza ya wazee mkoa na kuwaeleza wazee umuhimu wa mabaraza ya wazee na sifa za mtu kujiunga na mabaraza.
Katibu huyo wa Oganaizesheni Taifa amewataka viongozi kuwashirikisha wazee katika mambo mbalimbali ya maendeleo ili kuimarisha Chama na Serikali na kuweza kufanya urahisi wa utendaji kazi.
Pia amesema Chama hakitamvumilia mtumishi yeyote atakayewatendea uovu wazee katika maeneo ya upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii.
Akieleza changamoto zinazowakabili wazee mkoa wa Tanga mzee Mnyamisi amesema maradhi kwa wazee ni changamoto inayowatesa wazee kwani hawana kipato ni kidogo na kwa wanaopokea Pensheni haitoshelezi kutokana na gharama za matibabu
Naye mzee Salimu Kisauji ameiomba serikali kuwasaidia wakazi wa Tanga kupata Kiwanda cha kuchakata Samaki kwani kwa sasa uvuvi uko vizuri Tanga na samaki wapo wa kutosha.
Hata hivyo wazee kutoka Korogwe wameeleza kilio chao kwa benki ya posta (TCB) kushindwa kuwasaidia kukuza mitaji yao na badala yake kuwarudisha nyuma kwa riba zinazokatisha tamaa wazee kujiongezea kipato kwa miradi midogodogo ya kujikwamua
Akijibu hoja ya wazee katika baraza hilo mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewahakikishia wazee kupata huduma safi za afya na yeyote atakaye mfanyia ovu mzee atachukuliwa hatua za kisheria
huku Mwenyekiti CCM mkoa Tanga Rajab Abdallah akieleza kusikitishwa na kero ya afya kwa wazee na kuwataka wazee kutoa ushirikiano kwa Chama ili kutatua changamoto hiyoifike mwisho lengo likiwa kuwaenzi wazee hao pamoja na viongozi waliopita kwa Mazuri waliyofanya katika nchi hii.
Social Plugin