Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MCHENGERWA : SITAWAVUMILIA WANAOKWAMISHA MIRADI YA MAENDELEO

Na Mariam Kagenda - Kagera

Viongozi wa serikali katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamehimizwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika manispaa hiyo inatekelezwa kwa ufasaha kwani lengo la Rais wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Kagera inakuwa na maendeleo .

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh Mohammed Mchengerwa amesema hayo wakati wa hafla ya utiaji wa saini mikataba ya usanifu wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) kwa miji 15 ya kundi la pili.


Mhe Mchengerwa amesema kuwa  Rais Samia Suluhu Hassan  ameridhia kuletwa kwa miradi mikubwa ya maendeleo  katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na Soko,barabara  na stendi kwani anafahamu kuwa miradi hiyo ni  ndoto za muda mrefu za wana Kagera.


Amesema kuwa miradi hiyo mikubwa ni ndoto za vijana ,wazee,wtoto na wakina mama hivyo viongozi wanaoshiriki kusimamia miradi hiyo waisimamie kwa ufasaha ili iweze kutekelezwa kwa ufanisi kwani hatomvumilia mtu yoyote yule atakayekwamisha miradi hiyo.


Kwa upande wake mratibu wa mradi wa TACTIC ushiriano wa Bank ya Dunia Mhandisi Humphrey Kanyenye wakati akisoma taarifa ya mradi huo amesema kuwa mradi wa Tactic huo unagharamiwa  na serikali kuu kupitia mashart nafuu ya mkopo kutoka benk ya dunia na unatekelezwa kwa kipindi cha miaka 6.


Lengo la mradi huo ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa miji pamoja na kuziwezesha halmashauri za miji na majiji kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ambapo manispaa ya Bukoba imetengewa bajeti ya shilingi bilioni 23 .


Aidha katika fedha hiyo iliyotengwa miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni ujenzi wa stendi mpya ya Kisasa Kyakairabwa, ujenzi wa soko la kisasa ,ujenzi wa kingo za mto Kanoni na taa za barabarani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com