MKAZI wa Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Bernard Mwingira ameuaga umasikini baada ya kuibuka mshindi wa 'Jackpot' na kujinyakulia kiasi Cha Sh 250,000,000/= kupitia kampuni ya michezo ya kubashiri ya (BetwayTanzania).
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa hundi yenye kiasi hicho cha fedha katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana, Ndugu, Bernard Mwingira pamoja na mambo mengine amesema ushindi huo umempa faraja kubwa huku akiwataka wadau wengine wa mchezo huo kuiamini kampuni hiyo na kubashiri nayo kila wakati
"Sikutarajia kuwa ningeshinda kiasi hiki kikubwa cha fedha, nimekuwa nikishinda bashiri zangu nyingi ila siyo zenye kiasi kikubwa kama hiki cha fedha, ukweli najisikia furaha sana, nawasihi Watanzania wenzangu kuendelea kubashiri michezo mbalimbali ya kampuni hii ikiwemo Jackpot ili nao waweze kuwa washindi", amesema Ndugu. Bernard Mwingira.
Ndugu Bernard Mwingira aliyewasili Dar es Salaam juzi akitokea mkoani Ruvuma amesema kwake ushindi huo umekuja wakati mzuri hususani kipindi hiki ambacho ni msimu wa sikukuu huku akiahidi kuitumia fedha hizo kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kufanya biashara.
Ameushukuru uongozi wa kampuni hiyo ya (Betway Tanzania) kwa ushirikiano waliuonyesha tangu aibuke na ushindi huku akisisitiza kuendelea kubashiri zaidi na zaidi kupitia kampuni hiyo kwa kuwa inaaminika.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya (Betway Tanzania) Ndugu Calvin Mhina mbali na kumpongeza mshindi huyo amesema kampuni hiyo imekuwa karibu na wateja wake wakati wote huku akisisitiza kuwa ushindi na malipo kwa mshindi huyo ni kielelezo cha uaminifu wa kampuni hiyo.
Amesema wao kama kampuni Bora ya ubashiri Tanzania na Duniani kote ushindi huo unawafanya kuendelea kujiweka mbele zaidi hasa kwa kuwa na promosheni nyingi nzuri zinazomuwezesha mtu kushinda kwa urahisi.
Aidha Meneja Masoko huyo amesisitiza kuwa wao kama (Betway Tanzania) ndo kampuni pekee yenye Jackpot kubwa Zaidi maarufu lkwa jina Billionea Jackpot inayoweza kumpatia mshindi Billion 5 kwa shillingi 500 tu kwa ajili ya kuwawezesha watu wengi kushinda kwa kuwa ndiyo malengo yao kuona watu wengi zaidi wakishinda.
Social Plugin