Je unahitaji vifungashio!! Karibu katika Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio Rafiki kwa Mazingira 'AZAT' kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Karibu sana ujipatie vifungashio vyetu rafiki kwa mazingira na vyenye ubora wa hali ya juu!! Tayari vipo sokoni ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vifungashio pamoja na kutunza mazingira.
“Katika kiwanda hiki cha AZAT tunatengeneza vifunganishio rafiki kwa mazingira kwa kutumia karatasi ngumu na bora. Kwa sasa tuna vifungashio aina tano na tunatengeneza kulingana na mahitaji ya mteja ,kuanzia robo kilo hadi kilo tano. Vifungashio hivi havilowani haraka. Hata ukihitaji nembo ya Biashara yako tuiweke, tunakuwekea kwenye vifungashio”,anasema Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio Rafiki kwa Mazingira 'AZAT' Mhe. Azza Hilal Hamad.
“Tunawakaribisha sana wadau wetu wakiwemo wafanyabiashara , wajasiriamali na wananchi wote. Vifungashio hivi ni bora na vigumu, vinafaa kutumika kufungia bidhaa kwenye maduka ya dawa za binadamu, dawa za mifugo, Super Market, wauza chips, mama lishe, wauza matunda, Hotelini n.k”,ameongeza.
Amesema kwa yeyote anayehitaji vifungashio vya AZAT bidhaa tayari zipo kwenye maeneo mbalimbali au afike kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani Mjini Shinyanga au apige simu namba 0787653394
Social Plugin