Washiriki wa mbio za kuhamasisha kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wakijiandaa kuanza mashindano
Washiriki wa mbio za baiskeli kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa na mgeni rasmi na Maofisa Waandamizi wa Barrick Bulyanhulu.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Jackson Oswago, akiongea katika maadhimisho hayo.
Kaimu Meneja wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Abdallah Kipara,akiongea na Wananchi wa Msalala.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Jackson Oswago,akikaribishwa na Maofisa Waandamizi wa Barrick katika maadhimisho hayo,
Wananchi wakifuatilia matukio katika kampeni hizo
Baadhi ya washiriki wa mbio za kuhamashisha kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wakipata zawadi kutoka kwa mgeni rasmi
Baadhi ya washiriki wa mbio za kuhamashisha kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wakipata zawadi kutoka kwa mgeni rasmi
****
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, umeungana na Serikali na wadau wengine kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo umeandaa kampeni ya kutoa elimu dhidi ya vitendo hivyo katika vijiji na shule zilizopo jirani na Mgodi huo.
Akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa kata ya Segese ,Halmashauri ya Msalala, Kaimu Meneja wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Abdallah Kipara, amesema kupitia kampeni wanafunzi mashuleni na wananchi kwa ujumla wataweza kupata elimu ya utambuzi wa ukatili wa kijinsia na hatua za kuchukua iwapo watafanyiwa vitendo hivyo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Jackson Oswago ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo katika wilaya hiyo ameishukuru Barrick Bulyanhulu kwa kuandaa kampeni hiyo ambayo alidai itachangia kuleta mabadiliko katika jamii na aliwaasa wazazi kuwa na muda maalumu wa kuzungumza na watoto wao ili kufahamu changamoto wanazopitia ili waweze kuwasaidia.
Mgodi wa Barrick Bulyahulu, kila mwaka inaungana na Serikali na wadau mbalimbali kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kwa mwaka utazifikia kata 4 ikiwa kata mbili ni kutoka halmashauri ya wilaya ya Msalala na kata mbili ni kutoka halmshauri ya Nyan’ghwale, mkoani Geita.
Social Plugin