Na Mwandishi wetu - Mwanza
Taasisi ya waandishi wa habari wa kuendeleza shughuli za bahari na uvuvi Tanzania (TMFD) imetoa mafunzo ya dhana ya uchumi wa buluu na faida zake kwa waandishi wa habari wa kuripoti habari za uvuvi na bahari Nchini.
Mafunzo hayo yalitolewa jana kwa njia ya mtandao ambapo kusudio kubwa lilikuwa ni kuwa kuwapa nafasi washiriki kujua dhana ya uchumi wa buluu na faida zake.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Edwin Soko alisema kuwa dhana ya uchumi wa buluu ni ngeni Nchini hivyo ni vizuri waandishi wa habari wakaijua na kujua faida zake ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa uchumi wa bluu..
" tunataka waandishi wa habari kwanza wajue vizuri maana ya uchumi wa buluu na pia waanze kuandika habari zao wakiwa tayari wana uelewa wa uchumi wa bluu" Alisema Edwin Soko.
Betty Mssanja Mwenzeshaji alisema kuwa, uchumi wa buluu una faida nyingi sana ikiwemo kujenga meli, kuvuna rasilimari za habari ikiwemo samaki wa mapambo, uvunaji wa madini majini, uchimbaji wa mafuta na utalii wa fukwe na faida nyingine nyingi.
Betty pia aliwataka waandishi wa habari kuwa wanaufaikaji wa uchumi wa bahari na wasiishie kuandika tu bali wanufaike kifedha kutokana na uchumi wa bluu.
Pia mafunzo hayo yaliweka maazimio ya waandishi wa habari wawe mabalozi wazuri wa uchumi wa buluu, pia wafikirie kuwa na miradi ya pamoja ya mfano kwenye eneo la uchumi wa buluu.
Jumla ya waandishi wa habari arobaini na mashirika yasiyo ya kiserikali matano walinufaika na mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yakiandaliwa na Taasisi ya waandishi wa habari wa kuendeleza shughuli za uvuvi Tanzania (TMFD) kwa kushirikiana na Mwanza Youth and Children Network pamoja na Taasisi ya blue economy, Acquaculture Tanzania .
Social Plugin