Mahafali ya tatu ya kidato cha nne ya shule ya Sekondari Little Treasures iliyopo Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Desemba 1, 2023 ambapo jumla ya wanafunzi 63 wamehitimu elimu ya kidato cha nne mwaka 2023 ambapo wavulana ni 30 na wasichana 33.
Akisoma risala ya shule kwenye mahafali hayo ,Mkuu wa shule ya Sekondari Little Treasures Alfred Mathias amesema wanafunzi hao walifundishwa na kuandaliwa vizuri katika taaluma ili waweze kukabiliana kikamilifu na mitihani ya taifa (NECTA) mwaka huu hivyo wanatarajia matokeo mazuri kwenye matokeo kama ilivyo kawaida ya shule hiyo.
“Tunapenda kuwafahamisha kuwa katika
matokeo ya mitihani ya mock shule yetu ilikuwa ya pili mkoa kati ya shule 154
na ya kwanza kwenye wilaya kati ya shule 26 kwa kufanya vizuri kwa kupata wastani wa daraja ‘A’, hii ni ishara nzuri
kwa mitihani yao ya taifa ambayo wameifanya kutoka tarehe 13 hadi
24/11/2013”, amesema Alfred Mathias.
Alfred Mathias
“Pia tunayo furaha kuwaarifu wazazi na walezi juu ya matokeo mazuri ya shule ya msingi Little Treasures katika mitihani ya kumaliza darasa la saba 2023 tumefaulu kwa wastani wa alama 46 ya 50 wanafunzi wote wameweza kupata wastani wa ‘A’ na kufanikiwa kuwa wa kwanza kwenye wilaya kati ya shule 56 na wa kwanza kwenye mkoa kati ya shule 658 katika kundi letu matokeo haya mazuri ni kwa ushirikiano mzuri kati yetu na wazazi/walezi kwa ushauri, michango na ada wanazotoa tunashukuru kwa ushirikiano wanaotupatia”, amesema Alfred Mathias.
"Kutokana na maendeleo ya teknolojia shule
imefanikiwa kufundisha masomo ya Kompyuta ili kuwapa wanafunzi elimu na ujuzi wa
kutumia kompyuta katika karne hii ya kidigitali lakini pia tunaushukuru viongozi
wa elimu mkoa, wilaya na kata kwa
ushauri na maelekezo yao katika masuala ya kitaaluma kulingana na miongozo ya serikali”, ameongeza Alfred
Mathias.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Meneja wa shule za
Little Treasures Wilfred Mwita amesema shule za Msingi na Sekondari Little
Treasures zimekuwa chachu kubwa katika sekta ya elimu katika mkoa wa Shinyanga na
taifa kwa ujumla huku akiahidi kuwa wataendelea kuboresha zaidi miundombinu ili
kuwawezesha shule wanafunzi kupata elimu yenye ubora na uhakika.
Wilfred Mwita
“Tunawashukuru
wazazi na walezi kwa kuendelea kutuamini sisi Little Treasures kuwa sehemu
sahihi ya kupata elimu yenye viwango bora, elimu tunayoitoa imekuwa chachu
kubwa katika sekta ya elimu ndani ya mkoa na taifa kwa ujumla”, amesema Wilfred
Mwita.
Lucy Mwita
Mkurugenzi
wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita amesema tangu
shule ya sekondari Little Treasures ilipoanzishwa imeendelea kufanya vizuri
kwenye mitihani ya taifa na imekuwa ikipata wanafunzi katika uwiano sawa kati
ya wasichana na wavulana na kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao ya
elimu ya juu na kuahidi kuja na mpango wa kuanzisha utoaji elimu ngazi ya juu ambayo
ni kidato cha 5 na 6 kwenye shule hiyo.
Naye Mgeni Rasmi Kaimu Meneja kutoka Benki ya NMB Shinyanga
Erick Marandu kwa niaba ya meneja wa benki hiyo ameipongeza shule ya sekondari Little
Treasures kwa maendeleo mazuri katika elimu na kuupa heshima mkoa huo kwa
kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa huku akiwasihi wanafunzi
hao waliohitimu kidato cha nne kutojihusisha na makundi yasiyofaa mara baada ya
kuhitimu masomo yao na kutoshiriki vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za
kulevya na uasherati.
Erick Marandu
Social Plugin