Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATAIFA MBALIMBALI YATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA WAFANYAKAZI WAHAMIAJI


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MATAIFA mbalimbali yametakiwa kuweka mazingira mazuri ya kuwafanya wafanyakazi wahamiaji wanapotoka kwenye nchi zao wanakuwa na mazingira rafiki wakati wanapofanya kazi zao ili kuepuka mkanganyiko kwenye kazi.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Cde Hery Mkunda wakati wa kikao cha Mtandao wa wafanyakazi wahamiaji wa Afrika unafanyika chini ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Kimataifa.

Amesema katika kikao hicho ambacho washiriki 32 kutoka nchi za Afrika wameshiriki na kujadili namna ya kuweka mfumo rafiki ambao utaakisi wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao.

"Sisi kama wafanyakazi kupitia shirikisho la wafanyakazi Afrika tumeona ni muda muafaka kuungana wote kwa pamoja kushirikiana kuona jinsi gani tunaweka mazingira katika nchi zetu kuhakikisha tunawalinda hawa wafanyakazi wanapata haki zao, wanalindwa na kuhakikisha kwenye ajira zao wanapata haki za msingi ". Amesema

Aidha amesema kuwa wafanyakazi wahamiaji ili aweze kupata haki zao za msingi anapotoka nchini Tanzania kwenda nchi nyingine lazima awe salama na kulindwa.

Pamoja na hayo ameipongeza Serikali kwa kuingia mkataba na nchi za Uarabuni ambao utawasaidia wafanyakazi wanaotoka Tanzania kwenda nchi za uarabuni na wao wa uarabuni kuja nchini Tanzania kuja kufanya kazi zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com