Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema taarifa zinazo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuahirishwa kwa maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) hakuhusiani na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuahirisha Maadhimisho hayo.
Maadhimisho hayo yalikuwa yafanyike Jijini Mwanza Desemba 16, 2023 ambapo Mhe. Rais aliridhia mwaliko wa CWT Novemba 14, 2023 kuwa Mgeni rasmi na baadae CWT waliomba kubadili tarehe ya maadhimisho ifanyike Desemba 13 badala ya tarehe aliyoridhia Mhe. Rais.
Prof. Ndalichacho amebainisha hayo Desemba 12, 2023 Jijini Dar es salaam ambapo amesema Mhe. Rais alielekeza wataarifiwe tarehe waliyoibadili atakuwa na jukumu lingine licha CWT kuendelea na maandalizi na kubadilisha hadi Desemba 16, 2023.
Aidha, Mhe. Ndalichako amewahakikishia walimu nchini kuwa serikali ya awamu ya Sita inatambua na kuthamini mchango wao na itaendelea kushirikiana na Wafanyakazi wote wakiwemo walimu ambao wanafanya kazi kubwa ya kuwalea na kuwajengea ujuzi watoto kwa ajili ya kujenga Taifa na ustawi kwa watanzania.
Social Plugin