Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi,akizungumza wakati akizindua Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu leo Desemba 1,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi,akisisitiza jambo wakati akizindua Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu leo Desemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Bw.Rasheed Maftah,akizungumza wakati wa Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu leo Desemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt.Simon Chacha akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu leo Desemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania Bara Ndugu Ernest Kimaya,akizungumza wakati wa Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu leo Desemba 1,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi (hayupo pichani) ,akizungumza wakati akizindua Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu leo Desemba 1,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi,akiwa katika picha ya pmoja mara baada ya kuzindua Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu leo Desemba 1,2023 jijini Dodoma.
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI inaendelea kuyapa kipaumbele masuala ya watu wenye ulemavu,kuwapenda,kuthamini haki na ustawi wao kwa kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo, kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2004.
Hayo yamesemwa leo Disemba 1,2023 jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi,wakati akizindua Kongamano la Kujadili Mada mbalimbali kuhusu Watu Wenye Ulemavu kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu
“Lengo kuu la kongamano hili ni kujadili mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalam wetu na kuweza kutoa michango yetu pamoja na kushauri namna bora ya kuboresha huduma hizo katika maeneo hayo husika. Aidha, nimejulishwa kuwa mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Afya ya akili, ujumuishwaji wa masuala ya afya kwa Watu wenye Ulemavu pamoja na afya ya uzazi, fidia kwa Wafanyakazi wanaopata ulemavu kazini, Huduma kwa Watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi pamoja na mfumo wa utolewaji taarifa kwa Watu wneye Ulemavu”
Na kuongeza kuwa “Serikali inaendelea kukamilisha kuandaa Mwongozo wa Ufikivu wa miundombinu, Mwongozo wa uanzishwaji, uendeshaji na usimamizi wa vyuo vya ufundi stadi na marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vya Serikali na watu binafsi pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu katika jamii,” amesema Mhe.Katambi
Aidha Mhe.Katambi amesema kuwa wamefanya Maboresho ya miundombinu katika vyuo sita vya ufundi stadi na marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vilivyopo Yombo – Dar es Salaam, Sabasaba – Singida, Masiwani –Tanga, Luanzari –Tabora, Mtapika – Masasi na Mirongo- Mwanza na sasa upanuzi wa chuo hicho unafanyika katika eneo la Kisesa ikiwemo Ujenzi wa vyuo vipya vitatu katika Mkoa wa Ruvuma, Songwe na Kigoma.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, watu milioni 3.2 sawa na asilimia 9.3 ya watu milioni 44.9 wakati huo walikuwa na aina fulani ya ulemavu. Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 idadi ya Watu ni 61,741,120 hivyo inatarajiwa pia idadi ya Watu wenye Ulemavu kuongezeka ikizingatiwa ushirikishwaji wa Watu wenye Ulemavu ulikuwa mkubwa na hivyo kuongeza hamasa ya kushiriki.
Kongamano hilo limewashirikisha watendaji kutoka Idara za serikali na Taasisi zake, mashirika na taasisi zinazotoa huduma kwa Watu wenye Ulemavu, vyama vya Watu wenye Ulemavu, Watu wenye Ulemavu pamoja na vyombo vya habari. Ninatambua kuwa ninyi nyote ni wadau muhimu katika kongamano hili la leo ambalo linaenda kuangazia sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, ajira, uwezeshwaji wananchi kiuchumi pamoja na huduma kwa Watu wenye Ulemavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Bw.Rasheed Maftah, amesema kuwa zoezi la mapitio ya sera ya Maendeleo ya watu Wenye Ulemavu limeanza
''Zoezi hilo ni shirikishi kwani katika timu inayofanya mapitio ya sera hiyo imejumuisha Makundi yote ikiwemo Kamati za watu Wenye Ulemavu kuanzia ngazi ya Mtaa.''amesema Bw.Maftah