Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe.Dadi Kolimba akifungua semina ya EWURA kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Madiwani, Watendaji wa Serikali za mitaa na wenyeviti wa vijiji vya Wilaya hiyo kuhusu masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji, mjini Karatu, leo 19 Desemba 2023.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Mha. Lorivii Long’idu, akitoa mada kuhusu Udhibiti, kwenye semina kwa Viongozi wa serikali wilaya ya Karatu. Semina hiyo iliwahusisha Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Watendaji wa Serikali za Mitaa, Viongozi wa Vijiji na taasisi mbalimbali.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe.Dadi Kolimba (hayupo pichani) akifungua semina ya EWURA kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Madiwani, Watendaji wa Serikali za mitaa na wenyeviti wa vijiji vya Wilaya hiyo kuhusu masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji, mjini Karatu , leo 19 Desemba 2023.
...........
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Dadi Kolimba, amewakumbusha viongozi wa taasisi, mamlaka na kampuni zinazotoa huduma za nishati na maji wilayani Karatu kuhakikisha wanatatua kero za wananchi, kutoa huduma kwa ufanisi, tija na kuwapa taarifa sahihi wadau wake.
Mhe. Dadi ameyasema hayo leo, wakati akifungua semina ya EWURA kwa viongozi wa Wilaya ya Karatu kuhusu shughuli za kiudhibiti na wajibu wa viongozi katika kuboresha huduma na kuwasihi kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi kwa wakati.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini Mha. Lorivii Long’idu amesema, EWURA ina utaratibu rasmi wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wateja wa huduma za nishati na maji na ipo tayari kushirikiana na wadau kuhakikisha malengo ya Serikali ya kuboresha huduma kwa Watanzania yanatimia.
Social Plugin