Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAHARAKATI WA JINSIA KUTOKA TGNP WABAINI SABABU ZINAZOCHANGIA WANAWAKE KUTOPEWA UONGOZI RUANGWA


WANAHARAKATI wa jinsia kutoka mtandao wajinsia nchini (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la (UN Women)Wanaendesha Mradi katika Kata ya Mandawa Halmashauri ya Ruangwa wenye lengo la la kutambua ushiriki wa Wanawake katika Uongozi na kujua wanawake wana nafasi gani katika mgawanyo wa mali na umiliki wa rasilimali.

Akizungumza na waandishi wahabari Desemba 18,2023 Mwanaharakati wa Jinsia Bi.Scola Makwaiya amesema kuwa wapo katika eneo hilo kwa ajili ya kutambua ushiriki wa Wanawake katika Uongozi,na kuona wanawake wana nafasi gani katika mgawanyo wa mali na umiliki wa rasilimali.

"Kwahiyo tupo hapa kwa mambo mawili kuona hali ya ushiriki wa Wanawake katika Uongozi ungozi tukisema ungozi ni Uongozi wa kiserikali na Uongozi wa kijamii lakini pia tunataka kujua namna gani ya mgawanyo wa rasilimali kwa maana haki za uchumi kufikia kumiliki na mgawanyo wa rasilimali kwa ngazi wa kaya pia ngazi ya jamii"Bi Scola Makwaiya Amesema.

Aidha amesema kuwa walengwa wa Mradi huo ni Wasichana,wanawake na wanao ishi na ulemavu na ameeleza kwamba wameanza zoezi lao kwa kukutana na wananchi kuanzia siku ya Jumanne hadi siku ya Jumamosi ambapo wametambua changamoto zinazo sababisha wanawake wasiwepo katika Uongozi nasababu zinazo sabisha wanawake wasiweze kuwa na haki zao za kiuchumi.

Amesema mambo ambayo yamejitokeza ambayo ni vikwazo katika suala la mwanamke asiweze kupewa nafasi ya Uongozi ni mazoea ya kuona mwanamke hawezi kuwa kiongozi pamoja na suala la imani.

"Maeneo haya wengi ni dini ya kiislamu ndio imetawala sana na moja ya imani ya dini kiislamu inasema mama ni mwanamke anapaswa kukaa nyumbani azae watoto alee kwa maana kwamba sio sahihi mwanamke kuwa ni kiongozi kwa upande mwingine imeonekana ni wivu kwamba akifanya kazi atamdharau kiongozi",Bi Scola Amesema

Pamoja na hayo amebainisha kuwa uwezo wa kiuchumi nao umekuwa ni kikwazo kwa wanawake kuwa kiongozi pamoja na suala la Rushwa ambapo mwanamke analazimika atoe rushwa ya ngono na kifedha kwa kuandaa zawadi kwa wananchi ili apate nafasi kuchaguliwa kuwa kiongozi.

TGNP imekuwa ikitoa elimu kwa jamii kuhusu usawa wa kijinsia na kupiga vita mfumo dume ambao umekuwa ukiwa tenga Wanawake na wasichana kwa kuto toa fursa sawa katika masuala mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com