WANANCHI WA PERA NA BWILINGU WASHUKURU UTEKELEZAJI MRADI WA LTIP




Na Alex Sonna-CHALINZE

WANANCHI wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani wamepongeza serikali kwa utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Miliki za Ardhi (LTIP) unalenga kupanga, kupima na kurasimisha maeneo yao.


Mmoja wa wananchi wa Kata ya Pera, Paul Legeza, amepongeza mradi huo umekuwa shirikishi ikiwamo kuacha maeneo ya barabara.

Oliver Kinambale, amesema kabla ya mradi kulikuwa na migogoro mingi ya ardhi na sasa upimaji huo umesaidia kuondokana na hali hiyo iliyokuwa ikiwakwamisha kimaendeleo.

“Migogoro ilikuwa inazuia magari kupita kutufikia kwenye makazi yetu kwasasa barabara zipo, wito wangu kwa serikali tunaomba maeneo ambayo hayajafikiwa na upimaji yafikiwe,”amesema.
Mwenyekiti wa Urasimishaji wa ardhi Chalinze Kata ya Pera, Adam Kiponzile, alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea mradi huo ambao umepokelewa kwa shangwe na wananchi.

“Tunawashukuru wataalamu walikuwa wanatueleza hatua kwa hatua, wananchi wameelimishwa na wameupokea,”amesema.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ramadhan Possi, ameshukuru serikali kwa utekelezaji wa mradi huo na kuifanya Chalinze kuwa miongoni mwa Halmashauri 41.


“Mradi huu tumeona tuanze Mamlaka ya Mji mdogo kwenye kata hizi mbili Pera na Bwilingu, tunashukuru serikali kwa mradi huu maeneo yalikuwa hayana mpangilio yalisababisha migogoro mingi, mradi huu utaboresha makazi yetu na unafaida kubwa sana,”amesema.


Amesema Wilaya hiyo ina kata 15 na kuomba kupitia mradi huo kuendelea kusaidia kupanga, kupima na kurasimisha maeneo ya wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post