Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kampuni ya Dhahabu ya Barrick imekabidhi jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege lililojengwa kwa gharama ya shilingi Milioni 896.7 katika Uwanja wa Ndege wa Mgodi uliofungwa wa Buzwagi katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Akizungumza leo Jumapili Januari 21,2024 wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo hilo, Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow amesema jengo hilo walilolikabidhi kwa serikali ya Tanzania litahudumia zaidi ya abiria 200 kwa wakati mmoja ikilinganishwa na abiria 25 tu hapo awali.
Amesema jengo hilo jipya la abiria lililogharimu jumla ya shilingi Milioni 896.7 linalojumuisha sehemu ya kuwasili na kuondoka, sebule ya watu mashuhuri na chumba cha mikutano, duka la kahawa na zawadi, huduma kwa watu wenye ulemavu linatarajiwa kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi katika wilaya ya Kahama.
“Hafla hii inaashiria kuhitimishwa kwa ubia wa miezi nane kati ya Barrick na TAA uliogharimu jumla ya Dola za Kimarekani 384,000, gharama iliyogawanywa baina ya Barrick tuliotoa dola 268,000 sawa na Shilingi za Kitanzania 615.8 na (70%) na TAA wametoa dola 116,000 sawa shilingi za Kitanzania Milioni 255.8 (30%) na utafungua fursa ya kuwa na huduma ya ndege yenye ratiba maalum kuja na kutoka Kahama”,ameeleza Bristow.
“Jukumu la Kampuni endelevu ya uchimbaji madini si kutengeneza thamani kwa wadau wakati uliopo bali pia ni kuhakikisha kuwa inaacha urithi mzuri ambao utaendelea kuhudumia jamii kwa muda mrefu baada ya uchimbaji kufikia mwisho katika mgodi wa Barrick Buzwagi”,amesema Bristow.
Bristow ameongeza kuwa ,Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi ulikuwa kitovu cha uchumi wa mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania kwa takribani miaka 15 ambapo katika kilele chake, Buzwagi ulikuwa mgodi wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania na uliajiri watu 3000 na maisha yake ya uendeshaji yalifika tamati Julai 2021 na mgodi huo ulifungwa rasmi Julai 2022.
Amesema tangu 2022, Barrick imekuwa ikishughulikia ukarabati wa mazingira ya Buzwagi huku ikiendeleza mipango yake ya kuubadilisha mgodi wa Buzwagi kuwa ukanda maalumu wa kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha funguo za jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege Kahama
Naye Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inathamini kazi kubwa inayofanywa na Wawekezaji na imeendelea kuweka mazingira Rafiki kwa wekezaji ili kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi wote.
“Barrick ni wadau wakubwa wa serikali, tumekuwa na ushirikiano mzuri na nyinyi na matunda yanaonekana, haya yote yanatokana na mazingira safi ya uwekezaji yaliyowekwa na serikali ya Tanzania. Tunathamini sana kazi kubwa mliyofanya kukamilisha ujenzi wa jengo hili na tunaahidi litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo”,amesema Mhe. Mndeme.
“Tunashukuru kwa kutukabidhi jengo hili la uwanja wa ndege Kahama, tunaishukuru Barrick kwa uwekezaji huu, matarajio yetu ni kwamba uwanja huu wa ndege utaenda kuwa kiunganishi kikubwa cha nchi ya Tanzania nan chi jirani, tutahakikisha tunauboresha uwe wa kisasa zaidi ii ndege kubwa ziweze kutua hapa”,ameongeza Mhe. Mndeme.
Mkuu huyo wa Mkoa pia ametumia fursa hiyo kuikaribisha Kampuni ya Barrick kufanya utafiti wa madini katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga na kufanya uwekezaji kwenye sekta zingine.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir amesema ujenzi wa jengo hilo lililojengwa na Kampuni ya Umoja and Sons Ltd, ulioanza tarehe 01.03.2023 na kukamilika 30.11.2023 ukiwa na uwezo wa kubeba abiria 200 umekamilika kwa 100% ukigharimu shilingi Milioni 896.7 na kwamba wanategemea uwanja huo wa ndege utaongeza idadi ya abiria.
Ameongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, TAA itajenga eneo la maegesho ya magari,kununua samani, kufunga mfumo wa TEHAMA, mfumo wa ufuatiliaji wa mifumo ya usalama na kufunga mitambo ya kisasa kwa ajili ya ukaguzi wa mizigo na abiria.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiteta jambo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara (kulia).
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema Serikali imeendelea kuboresha viwanja vya ndege nchini vikiwemo vya Shinyanga, Mara, Tabora, Tanga, Mbeya, Arusha na Rukwa na ili uwanja wa Kahama uweze kupokea ndege kubwa unatakiwa kuongeza njia ya kuruka kwa ndege kutoka Km 1.5 hadi KM 2 jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wao ikiwa ni pamoja na kuweka lami.
“Uwanja huu wa ndege Kahama utaleta watu wengi Kahama. Uwanja ni sehemu ya kuongeza uwezo katika kuboresha usafiri wa anga nchini”,amesema.
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema Barrick imeunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya usafiri nchini na usafiri wa anga ikiwa ni mwendelezo wa wadau wa maendeleo kuunga mkono serikali kuboresha usafiri wa anga.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Jimbo la Kahama, Mhe. Jumanne Kishimba ameishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuwezesha ujenzi wa jengo la kisasa la abiria hali ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya usafiri wa anga wilayani Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akikata utepe wakati Kampuni ya Dhahabu ya Barrick ikikabidhi jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Mgodi uliofungwa wa Buzwagi katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) leo Jumapili Januari 21,2024. Wa kwanza kulia ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow, wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) baada ya kukata utepe wakati Kampuni ya Dhahabu ya Barrick ikikabidhi jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Mgodi uliofungwa wa Buzwagi katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) leo Jumapili Januari 21,2024. Wa kwanza kulia ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow akizungumza wakati akikabidhi funguo za jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow akikabidhi funguo za jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kushoto)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha funguo za jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha funguo za jengo jipya la uwanja wa ndege wa Kahama
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow akisaini nyaraka za jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir (kulia) wakisaini nyaraka za jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir (kulia) wakisaini nyaraka za jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir (kulia) wakibadilishana nyaraka za makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir (kulia) wakibadilishana nyaraka za makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiteta jambo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la uwanja wa ndege wa Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amir akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Meza kuu wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Rebecca Stephen akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Rebecca Stephen akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akimkabidhi barua maalum Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakifurahia jambo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mhe. Jumanne Kishimba akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akikabidhi Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow zawadi kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
Picha ya kumbukumbu
Picha ya kumbukumbu
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akiteta jambo na viongozi mbalimbali
Viongozi mbalimbali wakiwa katika uwanja wa ndege Kahama
Viongozi mbalimbali wa Barrick wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama. Kulia ni Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido
Viongozi wa Barrick na wadau wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Viongozi wa Barrick na wadau wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Wadau mbalimbali wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Viongozi mbalimbali wakitembelea jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow wakitoka katika jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow, Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Rebecca Stephen na Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido wakiwa katika uwanja wa ndege Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kushoto) na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow wakiwa katika uwanja wa ndege Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kushoto) na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow wakiwa katika uwanja wa ndege Kahama
Muonekano wa sehemu ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Muonekano wa sehemu ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Muonekano wa sehemu ya jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipanda ndege katika uwanja wa ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akijiandaa kupanda ndege katika uwanja wa ndege Kahama
Moja ya ndege ikiwa katika uwanja wa ndege Kahama.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin