Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RUWASA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI KISHAPU, DC MKUDE AMSHUKURU RAIS SAMIA, KAMAZIMA ASISITIZA 'HAKUNA MAJI YA BURE'

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu umeendesha Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira.

Mkutano huo umefanyika leo Ijumaa Januari 5,2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maji wilayani Kishapu ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo, Mhe. Mkude ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi wa Kishapu ambapo fedha nyingi zimewekezwa kwenye sekta ya maji.

Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kutuletea miradi ya maji yenye pesa nyingi. Tunaipongeza sana serikali kwa kutuletea maji Kishapu, hivi sasa hali ya upatikanaji wa maji inaridhisha tofauti na miaka ya nyuma”,amesema Mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude.

Aidha Mkude amewataka wananchi kulinda na kutunza miradi akisisitiza kuwa ni jukumu la kila mwananchi kutunza miradi ya maji.

Ni jukumu letu kuhakikisha miradi hii inatunzwa. Mtu yeyote anayehujumu miundombinu ya maji achukuliwe hatua, tusimuonee huruma mtu yeyote anayeharibu miradi ya maji. Tuendelee kutunza miradi hii kwani ni rasilimali muhimu sana duniani inayozidi hata mafuta”,ameongeza.

Katika hatua nyingine amewakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia huduma za maji na kuachana na mtazamo hasi kwamba huduma ya maji inatolewa bure.

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima amesema lengo la mkutano huo ni kuwaleta pamoja wadau wa maji katika Wilaya ya Kishapu ili kuweza kutathmini, kubadilishana uzoefu na kujadili mafanikio na changamoto katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Matumizi ya maji hayana mbadala hivyo sisi sote tunalo jukumu la kutunza mazingira ili vyanzo vya maji visiharibiwe, laikini pia tunalo jukumu la kutunza miundombinu ya maji kwenye maeneo yetu ambapo miradi ya maji inajengwa ili iweze kuwa endelevu na kutoa huduma ya maji kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na tunalo jukumu la kuchangia gharama za uendeshaji na matengenezo ya skimu za maji kwenye maeneo yetu, ili huduma ya maji endelee kupatikana muda wote”,amesema Mhandisi Kamazima.

Aidha amewaomba wadau wa maji wote wakawe mabalozi wazuri kwa wananchi hasa kwa suala ya kuchangia gharama za uendeshaji na matengenezo ya skimu za maji.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima 

Ukweli ni kwamba hakuna maji ya bure kama ilivyozoeleka kwa wananchi wetu kwa sababu uzalishaji wa maji unahitaji gharama kama vile gharama za umeme na madawa, kwa hiyo lazima kuchangia gharama hizi ili miradi yetu iweze kuwa endelevu na kutoa huduma kwa wananchi wetu”,amesema Mhandisi Kamazima.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akishauri kuwe na ushirikiano wa karibu kati ya viongozi katika kutunza miradi ya maji

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela ametahadharisha wanaotoboa mabomba ya maji kwamba yana Presha kubwa (mgandamizo mkubwa) wasijaribu kufanya michezo hiyo ili kuepusha majanga.

“Naomba viongozi tuchukue hatua kwa wananchi wanaoharibu miundombinu ya maji ili kuepusha majanga yanayoweza kujitokeza mfano watu kupoteza maisha lakini pia sisi kupata hasara”,amesema Mhandisi Payovela.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela
 
Mhandisi Payovela pia amehamasisha watumiaji wa huduma za maji kulipia ankara za maji kwa wakati huku akiwashauri wananchi watumie maji safi na salama kupitia miradi ya maji.

"Naomba tuhimize wananchi kutumia maji safi na salama yaliyotengenezwa kupitia miradi ya maji",amesema Payovela.

Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kishapu (OCD), Esther Gesongwe ameitaka RUWASA na wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pindi zinapojitokeza changamoto ikiwemo uharibifu wa miundombinu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joel Ndettoson  ametaka viongozi wa vijiji na kata kuwa na ushirikiano katika kuwabaini watu wanaoharibu miundombinu ya maji na kuwachukulia hatua za kisheria.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala ameagiza watendaji kushughulikia wote wanaoharibu miundombinu ya maji kwani ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha miundombinu inalindwa na kutunzwa huku akiziomba taasisi zenye madeni kulipia huduma ya maji.

Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge amesisitiza suala la kutunza na kulinda miundombinu ni wajibu wa kila mwananchi.

Nao washiriki wa mkutano huo wameomba mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua kali wale wanaoharibu miundombinu hususani katika eneo la Ng'wang’holo na Busongo ambapo mabomba yamekuwa yakiharibiwa na wananchi.

Pia wameshauri kuwa wananchi wanapaswa watambue kuwa miradi ya maji siyo ya serikali bali inatokana na wananchi wenyewe waitunze ili iwe endelevu.

Pia acheni kuchanganya siasa kwenye mambo ya maji, mtu aharibu miundombinu ya maji anakamatwa halafu anakuja mtu anasema huyu ni mpiga kura wangu muachie, hii hapana”,amesema Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza leo Ijumaa Januari 5,2024 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira. Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA Kishapu.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Wadau wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Meza kuu wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Kishapu, Godfrey Mbussa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joel Ndettoson akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Kishapu, Gven Noah akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kishapu (OCD), Esther Gesongwe akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu 

Wadau wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa wadau wa maji Wilaya ya Kishapu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com