Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMUUA MKEWE KWA KUMKATA KATA VIPANDE VIPANDE

Mkazi wa kijiji cha Dombwela wilayani Makete mkoani Njombe Juma Kyando (36) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe kwa tuhuma ya kumuua mke wake aitwaye Tumaini Luvanda (35) kwa kumkata panga na kumtenganisha viungo vya mwili wake na kisha kuvitupa mtoni.

Mkuu wa upelelezi mkoa wa Njombe, Joseph Mwalongo akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mhusika wa mauaji hayo.

Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwenyekiti wa mtaa wa Dombwela Joseph Mbilinyi wamesema mtuhumiwa huyo alikuwa anajihami kwa panga hivyo hakuna aliyeweza kumsogelea mpaka askari polisi walipofika eneo la tukio tayari alikuwa ameweka baadhi ya viungo vya mwili kwenye mfuko wa kiroba na kutupa kwenye mto uliopo jirani na nyumbani kwake.

"Tulianza kufuata alama za mfuko aliokuwa anavuta mpaka kwenye mto ndipo tukaona kiroba kikielea juu ya maji, tukakiopoa tukaanza kufuata mto,tukakiona kiungo kingine ambacho ni mbavu titi na shingo,tukaanza kutafuta kichwa hicho ndio kimetusumbua mpaka kukipata maana alitupa sehemu tofauti",ameeleza mwenyekiti wa mtaa.

Ndugu wa mtuhumiwa huyo, Medrick Kyando amesema kuwa ndugu yake hana historia ya kuwa na matatizo ya akili lakini anashangaa kuona ametekeleza tukio hilo la kikatili pasipo kujali watoto wanao waacha kwani ameacha watoto watatu ambao bado wana umri mdogo unaohitaji malezi ya wazazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com