Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na baraza la ushauri la wazee wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ,viongozi wa dini na machifu ili kujadili changamoto kadhaa zinazoukabili mkoa wa Shinyanga likiwemo suala la mmomonyoko wa maadili
Baadhi ya wazee, viongozi wa dini na machifu pamoja na wadau wengine walioudhuria kikao cha mkuu wa mkoa wa Shinynga katika kujadili changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa huo.
NA EUNICE KANUMBA-SHINYANGA
Mkuu wa mkoa wa shinyaga Christina Mndeme ametangaza kuanza kwa masako mkali ili kupamba na biashara ya ukahaba ambayo imeelezwa kukithri katika maeneo mbalimbali mkoani humo na kuwa kichocheo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili hususani kwa watoto kwani biashara hiyo imekuwa ikifanyika hata nyakati za mchana ambapo amesisistiza kuwa vita hiyo itawahusisha hata wananchi ambao wamekuwa wakiwahifadhi wanawake wote wanaofanya biashara ya kuuza miili yao.
Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 24 Januari mwaka 2024 katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa dini,machifu na baraza la wazeee la ushauri la manispaa ya Shinyanga lengo likiwa ni kujadiliana juu ya changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wa Shinyanga kwa sasa ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana uandikishaji hafifu wa wanafunzi wanaoanza masomo kwa mwaka 2024 pamoja na mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu.
"Wazee wangu tunakwenda kufanya masako kuanzia leo, kwa sababu bila kuchukua hatua kali kama mlivyoelezea hapa watoto wengine wanajifunza ,lakini mmeongea kwa uchungu sana kwamba wengine wanaanzia asubuhi wakati watoto wengine wanakwenda shule wanaangalia wengine usiku ,wengine mchana na wakati vitendo vya uhalifu vinaingia humo humo wizi ubakaji ulawiti na kwenda kinyume na maadili ya Kitanzania", amesema Mndeme.
Wakizungumzia maamuzi hayo ya serikali bssdhi ya wazee walioudhuria kikao hicho wameishukuru serikali kupitia Mkuu wa mkoa kwa uamuzi huo wa vita dhidi ya makahaba kwani utakwenda kukomesha kabisa biashara hiyo haramu ya ngono ili kulinda maadili ya mtanzania.
"Tunamshukuru sana mkuu wa mkoa kwa kuamua kuanzisha msako huo kwani utakuwa mwarobaini wa biashara hiyo haramu ambayo kwa sasa imekithiri sana na inafanyika kwa uwazi bila kujali kuwa kuna watoto amesema mzee Laurent Kashinje mjumbe katika baraza la wazee la ushauri la manispaa ya Shinyanga"
Social Plugin