Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TGNP YAWASILISHA UCHAMBUZI WA MISWADA YA SHERIA BUNGENI

Mkurugenzi Mtendaii wa TGNP, Lilian Liundi

Na Deogratius Temba, Dodoma

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamewasilisha maoni yenye mtazamo wa Kijinsia kwenve miswada mitatu ya sheria zinazoshughulikia masuala ya Uchaguzi kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, sheria na utawala Bora.

Miswada ambayo TGNP kwa kushirikiana na Vituo vya Taarifa na Maarifa na Washiriki wa semina  za Jinsia Maendeleo, wameipitia na kufanyia uchambuzi kwa mtazamo wa Kijinsia ni Mswada wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi 2023, Mswada wa Marekebisho va Sheria ya Vvama va Siasa 2023 na Mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka wa 2023 ambapo mbali na mapendekezo hayo.

TGNP Kama asasi inayotetea haki za Wanawake na usawa wa Kijinsia imesema kwamba, vifungu hivi vikipitishwa vitaenda kuboresha ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na nafasi Maamuzi, na kukuza demokrasia katika mchakato wa uchaguzi.

Katika mapendekezo, hayo pia TGNP imepongeza mswada wa Marekebisho va Sheria ya Vyama vya siasa kwa mara ya kwanza kwa kuingiza kifungu cha 13, ambacho kinaenda kuboresha Kifungu cha 10C cha sheria ya mwaka 2019, kwa kuweka sharti la kila chama kuwa na sera ya linsia na miongozo, kanuni sera zenye mtazamo wa Kijinsia.

Baadhi va Mapendekezo ambayo yamewasilishwa kwa Kamati ya Bunge kwa mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na Madiwani, Kifungu cha 6 (1),- Uteuzi wa wasimamizi wa Uchaguzi na watendaji wengine, kinachowapa wakurugenzi wa Mamlaka za serikali za Mitaa, kusimamia uchaguzi ambapo wamependekeza kifungu hicho kifutwe kabisa na kuwepo kifungu kinachoipa Tume nafasi va kuajiri wataalamu wake wenyewe.


Mkurugenzi Mtendaii wa TGNP, Lilian Liundi akiwasilisha mbele ya Kamati ameshauri kifungu cha 38(1 kinachoruhusu kuwepo kwa mgombea pekee ambaye anapita bila kupingwa kirekebishwe, na endapo,mgombea hana wenzake wa kugombea naye apigiwe kura ya ndio au hapana.

"Kifungu cha 38(1) kinaruhusu kuwepo kwa mgombea pekee, hii itaongeza ushawishi kwa matumizi ya pesa na rushwa kwa baadhi ya wagombea tunashauri kuweka sharti la kuhakikisha wagombea wa aina hiyo wanapigiwa, kura", alisema Bi. Liundi na kuongeza:

"Tunashauri, kusiwe na gharama za kupata kitambulisho cha kupiga kura endapo kimeharibika, kupotea, au kufutika, tunapendekeza kuondoa neno 'ada' matumizi va Vitambulisho mbadala kama vile NIDA.

Awali Mwenyeviti wa Kamati ya Kudumu va Bunge ya Utawala, Sheria na Katiba, Dkt. Joseph Kizito Mhagama, alisema kwamba, maoni ya TGNP yana kitu kipya kwa mtazamo wa Kijinsia na yataisaidia kamati kwa kiasi.

"Niwashukuru, sana ninajua ninyi ni wawakilishi wa asasi nyingi na makundi mbalimbali, muda umetubana maoni na mapendekezo yenu yote tunayafanyia kazi na na tutahakikisha tunapitia andiko lenu kwa umakini" alisema Dkt. Mhagama
Wanaharakati wakiwa na Mbunge wa Kishapu, Boniphace Butondo na Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa, Sisty Nyahoza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com