Mkurugenzi na Mwanzilishi wa taasisi ya Tupaze Sauti Foundation Agness Suleiman Kahamba akionesha tuzo
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa taasisi ya Tupaze Sauti Foundation Agness Suleiman Kahamba ameandika Historia ya kutunukiwa Tuzo ya miongoni mwa Wakurugenzi 100 bora Tanzania katika kipengele cha Wakurugenzi Bora wa taasisi zisizo na faida 2023/2024 'Not for Profit/MD of the Year zilizoandaliwa na kampuni ya Eastern Star.
Tuzo hizo zilizotolewa hivi karibuni Jijini Dar es salaam zina lengo la kutambua juhudi za mashirika 100 bora yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2023.
Agness Suleiman Kahamba kupitia taasisi ya Tupaze Sauti Foundation ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa katika kupaza sauti kutetea haki katika jamii kwa kushirikiana na serikali pamoja na taasisi binafsi alitangazwa mshindi wa Tuzo ya Mkurugenzi Bora wa taasisi zisizo na faida 2023/2024 'Not for Profit/MD of the Year.
"Ninayo furaha ya kupata Tuzo na kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wakurugenzi 100 bora Tanzania na mwanzilishi wa Taasisi isiyo ya faida 2023/2024 katika kipengele cha Not for Profit/MD of the Year kupitia taasisi ya Tupaze Sauti Foundation. Tuzo hii imetupa nguvu kubwa na chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kusaidia jamii kwa nguvu zote",amesema Agness Suleiman Kahamba.
"Tunawashukuru wadau wote wanaondelea kujitolea, kusaidiana na kushirikiana nasi katika kupambana na changamoto za jamii tunazokutana nazo",ameongeza
Social Plugin