Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kuhusu huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji alipotembelea Banda la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Januari 27,2024 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga linashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma wanazotoa ikiwemo Utoaji Pasipoti, Vibali vya Ukaazi, Vibali vya kuingia nchini (Visa),kudhibiti uhamiaji haramu, kuendesha kesi za uhamiaji haramu pamoja na kupokea maombi ya uraia.
PICHA na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin