AFISA MHIFADHI KANDA YA KUSINI ASHAURI WATANZANIA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII




Na Richard Mrusha _ Kitulo

AFISA Mhifadhi mkuu
 wa Kanda ya Kusini Jonathan Kaihura ametoa wito wa watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi zetu hapa nchini na hasa hifadhi ya Taifa ya Kitulo iliyopo katika mikoa ya  Njombe wilayani Makete na Mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe na Mbeya vijijini.

Amesema kuwa mara zote pamekuwa na dhana ya kwamba wanaopaswa kutembelea na kufanya utalii ni wageni kutoka nje ya Tanzania jambo ambalo si sawa hivyo ni vema wakajenga utamaduni wa kufanya utalii kwenye hifadhi mbalimbali hapa nchini .

Kaihura ametoa wito huo, Januari 22 ,2024  wilayani Makete wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambao wamejikita katika hifadhi ya Taifa ya Kitulo kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hiyo.

Akizungumzia hifadhi ya Taifa ya kitulo amesema hifadhi hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2005 na kwamba ni moja ya hifadhi muhimu ambayo inapatikana nyanda za juu kusini ambapo imezungukwa na mikoa miwili ambayo ni Njombe na Mbeya 

Amesema kuwa hifadhi ya kitulo ina vivutio vya kustajaabisha Saba, huku akitolea mfano uwepo wa Waterfall ambayo Maji yanatirirka msimu mzima, lakini pia kuna bustani nzuri sana ya  maua ambayo ni uoto wa asili lakini kubwa kuliko mandhari yake ni ya kipekee 

"Hapa Kitulo hakika Mungu ni wa ajabu sana na amepapendelea sana nadhan mmeona pale kwenye chanzo ambapo Maji yanatiririka msimu mzima na pamepewa jina la Mwakitelima ambaye ndiye alikuwa Mhifadhi mkuu wa kwanza katika hifadhi hii ya kitulo", amesema Kaihura. 

Ameongeza kuwa licha ya chanzo hicho lakini pia Kuna maporomoko ya msitu wa mto Nhumbe yote hayo yanapatikana katika hifadhi ya Taifa ya kitulo hivyo watanzania waje kutembelea vivutio hivyo watafurahi na wataburudika.

Amefafanua kuwa  hata gharama za kuingia kwenye hifadhi hiyo ni rafiki sana na hata sehemu za maradhi gharama zake ni rafiki sana ambapo kulala katika nyumba zilizopo kwenye hifadhi usiku mmoja ni sh.29000 tu lakini pia huduma za chakula vinywaji vyote vinapatikana ndani ya hifadhi.

Pia amesema ndani ya hifadhi hiyo pia Kuna wanyama kama swala na wanyama wengine lakini Kwa upande wa maua Kuna aina 45 za maua lakini pia Kuna mimea aina mbalimbali inapatikana hivyo ni fursa azmu Kwa watanzania kuendeleza kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za  kutangaza vivutio vilivyopo nchini Tanzania.

Hifadhi ya  Taifa ya kitulo ipo mita 2900 kutoka usawa wa bahari na inazunguka katika mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Njombe katika Wilaya ya Makete lakini pia katika mkoa wa mbeya na hasa mbeya vijiji pamoja Wilaya ya Rungwe Mhifadhi mkuu wa kwanza wa hifadhi hiyo alikuwa anaitwa Mwakilema .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post