Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kituo cha afya cha Bugarama kilichopo wilayani Msalala walipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kutoa zawadi za mwaka mpya kwa wagonjwa waliolazwa kituoni hapo na kwa wafanyakazi wa kituo hicho.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Everjoy Ngomamiti, (Mwenye miwani kulia) akikabidhi zawadi za mwaka mpya kwa Mganga mfawidhi , kituo cha afya Bugarama kilichopo wilayani Msalala , Beatha Alistide (kushoto) wakati wafanyakazi wa mgodi huo walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi mbalimbali za mwaka mpya kwa wagonjwa waliolazwa na wafanyakazi wa kituo hicho jana.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu.
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakigawa zawadi kwa baadhi ya wagonjwa na wafanyakazi wa kituo cha afya cha Bugarama.

**
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, uliopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga, umekabidhi zawadi za sikukuu za mwaka mpya 2024, kwa wazazi na wagonjwa waliolazwa kwenye kituo cha afya cha Bugarama ,sambamba na wafanyakazi wa kituo hicho.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Everjoy Ngomamiti, akiambatana na baadhi ya wafanyakazi walishiriki kugawa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa pamoja na kwa wafanyakazi wa kituo hicho.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Kaimu Meneja wa mgodi huo, Everjoy Ngomamiti ,alisema kampuni itaendelea kushiriki shughuli za maendeleo kwa jamii inayoishi kuzunguka mgodi huo sambamba na kuimarisha nao uhusiano mwema.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi , kituo cha afya Bugarama , Beatha Alistide ,alitoa shukrani kwa Barrick Bulyanhulu kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayozunguka mgodi, kusaidia kituo hicho kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi pia kutatua kutatua changamotombalimbali zinazojitokeza katika kituo hicho.