Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RUJAT YAKABIDHI CHETI CHA SHUKRANI TANAPA... WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KWA UKARIBU ZAIDI

Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT) kimetoa cheti cha shukrani kwa mamlaka ya uhifadhi nchini (TANAPA) kwa kutambua mchango wake uliowezesha kufanikisha kongamano la kimataifa la haki ya kupata taarifa 2023.

Akikabidhi cheti hicho kwa Kamishna wa Uhifadhi, Katibu wa RUJAT Prosper Kwigize ameeleza kuwa TANAPA ni mdau muhimu wa habari vijijini na RUJAT ilinufaika kwa kupata mchango uliosaidia kufanikisha kongamano lililoenda sambamba na mkutano mkuu wa wanachama.

Akipokea cheti hicho kwa niaba ya Kamshina mkuu wa uhifadhi nchini, Meneja wa TANAPA ofisi ndogo za Dodoma Kamishna Dr. Noelia Myonga ameshukuru RUJAT kwa kutambua mchango wa TANAPA katika sekta ya mawasiliano ya umma.

Dr. Myonga amesisitiza kuwa mamlaka ya uhifadhi iko tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa chama cha waandishi wa habari vijijini ili kutangaza shughuli za uhifadhi na manufaa yake kwa wananchi.

RUJAT kwa upande wake imejipanga kushirikiana na wadau wa maendeleo, mashirika ya umma, serikali na jamii kuhakikisha habari za maendeleo vijijini zinaandikwa na kutangazwa

Katibu wa Chama hicho Bw. Kwigize amebainisha kuwa hadi sasa RUJAT ina wanachama zaidi ya 100 wanaofanya kazi katika mikoa yote ya Tanzania Bara na kwamba idadi hiyo inatoa fursa ya habari za vijijini kuandika na kusikika kitaifa, kikanda na kimataifa.


Wakati huohuo RUJAT imetoa cheti kama hicho kwa Wakala wa Umeme vijijini REA pamoja na Shirika la Madini la serikali STAMICO.

Mashirika hayo ya umma yaliunga mkono kwa hali na mali katika kufanikisha kongamano la RUJAT mwaka 2023 lililokuwa na malengo ya kuhamasisha uandishi wa habari zenye tija na zinazogusa maslahi ya jamii vijijini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com