Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA MAJI MARYPRISCA MAHUNDI ATEMBELEA MIRADI YA MAJI LUSHOTO

Naibu Waziri wa Maji  Mhe. Maryprisca Mahundi amefanya ziara wilayani Lushoto kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji ukiwemo mradi wa Kijiji cha Kibohelo kata ya Magamba Wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Akiwa katika mradi huo Naibu Waziri Mahundi amewataka Wakandarasi kuhakikisha wanashiriki kutekeleza miradi hiyo hiyo na kumaliza kwa wakati ili kutoa huduma hiyo kwa wananchi.

Aidha Naibu waziri Maryprisca amemuagiza Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Wilaya Lushoto Erwen Sinzinga kuwachukulia hatua watumishi wawili wanaofanya uzembe katika mradi wa Nyankhei uliopo kata ya Ngulwi wilayani Lushoto

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com